Apr 21, 2023 11:17 UTC
  • Qatar na Iran zasisitiza uhusiano wa pande mbili na kuiunga mkono Palestina

Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuimarisha zaidi uhusiano na majirani ni katikia sera za kigeni za Tehran zinazopewa kipaumbele.

Rais Ibrahim Raisi amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani na kusisitiza kwamba, uhusiano wa Tehran na Doha ni katika mahusiano imara, thabiti nay a kirafiki katika eneo la Asia Magharibi ambayo ni mara chache kukumbwa na hali ya panda shuka.

Rais wa Iran sambamba na kutoa mkono wa kheri na Baraka kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya eidul-Fitr ameeleza kuwa, ustawi na maendeleo ya eneo la Asia Magharibi yanategemea mazungumzo na ushirikiano baina ya mataifa ya eneo hili.

Kadhalika amesisitiza juu ya udharura wa kuweko umoja na mshikamano baina ya mataifa ya Kiislamu ili kukabiliana na vitendo vya utawala ghasibu wa Israel ambao umekuwa ukifanya hujuma kila leo dhidi ya msikiti wa al-Aqswa.

Bendeza za Iran na Qatar

 

Kwa upande wake Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani naye ametoa mkono wa kheri na Baraka kwa serikali na wananchi wa Iran kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Mfunguo Mosi ambapo ameashiria pia uhusiano imara uliopo baina ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa, Qatar iko tayari kupanua ushirikiano wake na Iran katika nyanja zote.

Amir wa Qatar amelaani vikali pia uvamizi wa hivi karibuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na kusema, msimamo usiobadilika wa Qatar kuhusiana na kadhia ya Palestina ni kuwaunga mkono wananchi hao madhulumu.

Tags