Taathira ya Mapinduzi ya Kiislamu imeenea Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i967-taathira_ya_mapinduzi_ya_kiislamu_imeenea_afrika
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamepelekea kuwepo mwamko wa Kiislamu miongoni mwa watu wengi Afrika na hivyo kuwawezesha kuondoka katika mkwamo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 10, 2016 11:53 UTC
  • Taathira ya Mapinduzi ya Kiislamu imeenea Afrika

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamepelekea kuwepo mwamko wa Kiislamu miongoni mwa watu wengi Afrika na hivyo kuwawezesha kuondoka katika mkwamo.

Katika mahojiano na Shirika la Habari la Tasnim, Sheikh Mohammad Shoaib ambaye ni mwenyekiti wa wanafunzi Wanigeria katika vyuo vya kidini Iran ametathmini taathira ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran barani Afrika na kusema: "Kuwepo kiongozi mmoja ni nukta ambayo imeyapambanua Mapinduzi ya Kiislamu na mapinduzi mengine duniani."

Ameongeza kuwa: "Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran ni kiongozi wa kimaanawi ambaye anafungamana kikamilifu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu." Amesema Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran ameweza kuathiri nyoyo za watu wengi duniani kutokana na uchaji Mungu wake.

Shoaib amesema hata maadui wanakiri kuhusu nguvu na uwezo wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kwamba kundi lolote linalojiunga na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hupata mafanikio.

Mwanaharakati huyo wa Kiislamu kutoka Nigeria amebainisha kuwa maadui wanafahamu kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanakinzana na maslahi yao hasa kuwatawala kibeberu wanyonge duniani. Ameongeza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, chini ya uongozi wa Imam Khomeini MA, yalikuwa na taathira kubwa katika mwamko wa nchi za Afrika na kujikwamua nchi hizo kutoka katika satwa ya mabeberu.