Jasusi na kibaraka wa CIA, MOSSAD na SÄPO anyongwa nchini Iran
Hukumu ya kifo iliyotolewa na Mahakkama ya Iran dhidi ya Habib Farajollah Chaab, kiongozi wa kundi la kigaidi linalojiita Harakat al-Nidal, ambalo liliua makumi ya watu wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, kupitia mashambulizi kadhaa ya kigaidi nchini Iran, imetekelezwa leo asubuhi (Jumamosi).
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran Press, "Habib Farajullah Chaab" aliyepewa jina la utani "Habib Esyud", amekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Harakat al-Nidal tangu 2005 chini ya usaidizi wa mashirika kadhaa ya kijasusi, kama CIA, MOSSAD na SÄPO (shirika la ujasusi la Sweden) na baadhi ya nchi katika kanda ya magharibi mwa Asia; na kundi hilo la kigaidi chini ya uongozi wa Habib Asyud, limeua shahidi au kujeruhi zaidi ya raia 450 wa Iran.
Tarehe 22 Septemba mwaka 2018 pekee kundi hilo la kigaidi lilishambulia gwaride la polisi na jeshi katika mji wa Ahwaz kusini mwa Iran na kuua raia wasio na hatia wasiopungua 25. Wanachama wa kundi hilo walitangaza waziwazi kuwa ndio waliotekeleza hujuma hiyo ya kigaidi.
Harakati kubwa zaidi za kundi hili la kigaidi zilijikita katika operesheni za uharibifu, mauaji na milipuko ya mabomu katika eneo la Kusini Magharibi mwa Iran hususan mkoa wa Khuzestan, kuvuruga usalama na amani katika eneo hilo na hatimaye kushawishi wananchi kujitenga na Iran.
Habib Farajullah Chaab alikamatwa na vyombo vya usalama vya Iran nchini Uturuki Novemba 2020, na baada ya kukukamilika upelelezi na hatimaye kutolewa hati ya mashtaka, vikao nane vya mahakama vilifanyika vikishirkisha mawakili wake na mawakilishi wa familia za mashahidi wa mauaji hayo.
Habib Farajullah Chaab alikabiliwa na tuhuma za kufanya uharibifu katika ardhi kupitia njia ya kuunda, kusimamia na kuongoza kundi linalojiita Harakat al-Nidal al-Arabi na kupanga na kutekeleza mashambulizi ya kigaidi na uharibifu wa mali ya umma.
Farajullah Chaab amekiri kuwa na uhusiano na mashirika ya ujasusi ya Mossad na CIA. Kundi hilo pia limekiri kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh