Balozi wa Iraq aitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i97330-balozi_wa_iraq_aitwa_katika_wizara_ya_mambo_ya_nje_ya_iran
Balozi wa Iraq mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kufuatia kualikwa wanachama wa makundi yanayotaka kujitenga nchini Iran katika sherehe rasmi iliyofanyika katika eneo la Kurdistan nchini Iraq na kuendelea baadhi ya harakati za makundi ya kigaidi yaliyo dhidi ya Iran katika eneo hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 14, 2023 02:37 UTC
  • Balozi wa Iraq aitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Balozi wa Iraq mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kufuatia kualikwa wanachama wa makundi yanayotaka kujitenga nchini Iran katika sherehe rasmi iliyofanyika katika eneo la Kurdistan nchini Iraq na kuendelea baadhi ya harakati za makundi ya kigaidi yaliyo dhidi ya Iran katika eneo hili.

Mkuu wa Idara ya Kwanza ya Ghuba ya Uajemi katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, amebainisha malalamiko makali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu kualikwa wanachama wa makundi yanayotaka kujitenga na kuendelezwa harakati za baadhi ya makundi ya kigaidi huko Kurdistan ya Iraq, na kusisitiza kuwa hatua hiyo ni kinyume na makubaliano ya hivi karibuni ya usalama yaliyofikiwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq.

Magaidi hao wanaotaka kujitenga, kwa kujipenyeza ndani ya ardhi ya Iran na kujiunga na raia wa kawaida, wanaibua machafuko na pia kutekeleza miradi ya mauaji mara kwa mara dhidi ya watu wa Iran.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafahamu vizuri kuwa makundi hayo ya kigaidi yanaungwa mkono na utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi ikiwemo Marekani.

Kisheria na kwa kuzingatia kifungu cha 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa, Iran ina haki ya kufanya operesheni za kijeshi za upande mmoja dhidi ya magaidi hao wenye silaha.

Kwa kuzingatia hilo, vitengo vya makombora na ndege zisizo na rubani vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu vimeyalenga mara kadhaa makao makuu ya makundi ya kigaidi katika eneo la Kurdistan ya Iraq.