Kan'ani: Gurudumu la wakati haliende mbele kwa maslahi ya Marekani na Israeli
-
Nasser Kan'ani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema: Gurudumu la wakati haliendi mbele kwa maslahi ya Marekani na utawala haramu wa Israel.
Matamshi hayo yametolewa baada ya wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) kumchagua rais mpya wa Baraza Kuu la umoja huuo, ambapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechaguliwa kuwa mmoja wa makamu 21 wa rais wa Baraza Kuu.
Katika ujumbe wake wa Twitter leo Jumamosi, Nasser Kan'ani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, ameashiria mafanikio ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu katika Umoja wa Mataifa na kuandika: "Nchi ambayo imekuwa kitekeleza sera za ulimwengu wa kambi moja kwa miongo kadhaa na kudhoofisha mfumo wa kambi kadhaa, kutumia vibaya haki ya kura ya turufu kuunga mkono utawala wa kibaguzi wa Israel na kushusha hadhi ya Umoja wa Mataifa, imekasirishwa na hatua ya wanachama wa UN kuipigia kura Iran kushika nyadhifa katika Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesisitiza kuwa: "Gurudumu la wakati halisongi mbele kwa maslahi ya Marekani na Israel."
Katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, makamu wa rais ( manaibu) 21 huchaguliwa kwa ajili ya rais wa baraza hilo kwa kuzingatia kanda za kijiografia; wawakilishi 6 kutoka nchi za Afrika, wawakilishi watano kutoka Asia na nchi za Pasifiki, mwakilishi mmoja kutoka nchi za Ulaya Mashariki na wawakilishi 2 kutoka nchi za Amerika Kusini na Karibea, wawakilishi 2 kutoka nchi za Ulaya Magharibi na wawakilishi watano kutoka wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama wanachaguliwa kuwa makamu wa rais wa Baraza Kuu.