-
Iran: Mashirika 50 ya kijasusi yaliisaidia Israel katika Vita vya Siku 12 dhidi yetu
Oct 22, 2025 23:41Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran amesema: Katika vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel mwezi Juni mwaka huu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, adui alipanga kuzusha uvunjifu mkubwa wa amani nchini Iran na alijaribu kutumia magaidi wake wote wakufurushiaji walioachiwa huru huko Syria na Afghanistan kwa ajili ya kuvuruga usalama wa Iran ya Kiislamu lakini alishindwa. Mashirika 50 ya kijasusi yaliisaidia Israel lakini pia yalishindwa.
-
Iran: Hatutarudi kwenye meza ya mazungumzo hadi Marekani iachane na sera zake za kupenda makuu
Oct 22, 2025 23:11Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, sharti la kurejea Iran katika meza ya mazungumzo ni Wamarekani kuacha siasa zao za kijuba na za kupenda makuu.
-
Larijani aishukuru Russia kwa kuiunga mkono Tehran katika Baraza la Usalama
Oct 22, 2025 09:34Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amewasilisha kwa Russia shukrani za Jamhuri ya Kiislamu kutokana na hatua ya Moscow ya kuunga mkono msimamo wa haki za Tehran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mkabala wa hatua ya nchi za Magharibi ya kurejeshea hatua kali za kiuchumi dhidii ya Iran.
-
Iran yaidhinisha rasmi kujiunga na mkataba wa kupambana na ufadhili wa ugaidi
Oct 22, 2025 09:23Rais Masoud Pezeshkian amewasilisha rasmi sheria ya kujiunga Iran na Mkataba wa Kimataifa wa Kupambanana Ufadhili wa Ugaidi (CFT).
-
Iran yagundua maficho ya televisheni ya Israel inayoeneza uadui dhidi yake
Oct 22, 2025 02:47Operesheni ya kiintelijensia ya Iran iliyofanyika kwa mafanikio, imefichua waliko watu wanaohusika na shirika la kijasusi la Israel Mossad, ambao waliwatumikia maadui hasa Israel na Marekani wakati wa vita vya upashaji habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu Iran.
-
Larijani: Marekani haitaki Iraq iwe huru/ Baghdad: Usalama wetu na wa Iran ni kitu kimoja
Oct 22, 2025 02:46Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema: Ni lazima tufanye juhudi za kuzuia njama zozote zinazofanywa na watu baki wenye nia mbaya ya kuyaletea madhara mataifa ya Iran na Iraq.
-
Meja Jenerali Pakpour: Jahanamu itashuhdiwa iwapo Iran itashambuliwa
Oct 21, 2025 23:48Iran iko tayari kutoa jibu kali kwa uchokozi wowote endapo utafanywa dhidi yake katika siku zijazo. Ameyasema hayo Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye ametaharisha kuwa Iran "itaachilia moto wa kuzimu dhidi ya adui."
-
Msemaji wa serikali ya Iran: Azimio nambari 2231 limekwisha muda wake
Oct 21, 2025 23:08Fatemeh Mohajerani Msemaji wa serikali ya Iran amesema kuwa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililoidhinisha makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 limekwisha muda wake na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelitaarifu Baraza la usalama kuhusu kumalizika muda huo.
-
Teknolojia ya Nyuklia Yazaa Masuluhisho Mapya kwa Mustakabali wa Uchumi wa Iran
Oct 21, 2025 23:05Iran imezindua kituo cha kwanza cha mionzi ya kilimo katika eneo la kaskazini-magharibi, kilichopo Ardabil, hatua inayoonesha dhamira ya taifa kutumia teknolojia ya nyuklia kwa madhumuni ya amani ili kuimarisha usalama wa chakula na kukabili changamoto za kilimo kote nchini.
-
Kwa nini Afrika ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa Iran?
Oct 21, 2025 23:01Mkuu wa Jumuiya ya Biashara ya Pamoja ya Iran na Afrika amesema: "bara la Afrika ni hazina iliyofichika ya uchumi wa dunia na fursa kubwa kwa Iran."