-
Mawaziri wa mambo ya nje wa Misri na Kuwait wakaribisha mazungumzo kati ya Iran na Marekani
Apr 14, 2025 03:13Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amezungumza na mawaziri wenzake wa Misri na Kuwait na kuwaeleza kuhusu msimamo wa Tehran juu ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana iliyofanya na Marekani.
-
Kiongozi Muadhamu: Adui amekatishwa tamaa na ana hofu na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu
Apr 13, 2025 10:21Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Ali Khamenei leo Jumapili mchana amekutana na baadhi ya makamanda wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mnasaba wa Mwaka Mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia na kusisitiza kuwa, adui amekata tamaa vibaya na amekasirishwa na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu. Wakati huo huo amesisitiza kwamba, pamoja na kuwepo mapungufu, lakini kuna maendeleo pia yamepatikana, inabidi hayo nayo tuyaone.
-
Iran: Tunafanya mazungumzo na Marekani kuhusu kadhia ya nyuklia tu
Apr 13, 2025 10:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, tunapoangalia mawasiliano ya maandishi yaliyofanyika tangu mwanzo wa mchakato uliopelekea kufanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati yetu na Marekani tutaona kuwa, msingi wa mawasiliano hayo haukuwa na chochote kingine ghairi ya suala la nyuklia.
-
Iran yaitaka UN kutumia uwezo wake kusitisha mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza
Apr 13, 2025 07:26Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameuhimiza Umoja wa Mataifa kutumia uwezo wake wote kusimamisha mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi yake dhidi ya watu wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Iran yalaani shambulizi la kinyama dhidi ya raia wa Pakistan
Apr 13, 2025 06:59Ubalozi wa Jamhur ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan umelaani shambulio la woga dhidi ya kundi la raia wa Pakistan katika mkoa wa Sistan- Baluchistan.
-
Iran yaanza kutoa kadi za benki kwa wageni kutoka nje
Apr 13, 2025 02:54Benki za Iran zimeruhusiwa kutoa kadi za benki kwa wageni wanaotembelea nchi huku kukiwa na juhudi za kuimarisha utalii.
-
Iran: Mazungumzo ya Oman ni chanya na ya matumaini; kuendelea wiki ijayo
Apr 12, 2025 23:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi ameitaja duru ya kwanza ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekani kuwa "chanya na yenye kuleta matumaini."
-
Wizara: Iran imezalisha mifumo ya ulinzi zaidi ya 900
Apr 12, 2025 22:51Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema sekta ya ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu imeunda zaidi ya mifumo 900 ya ulinzi na zana za kijeshi; hatua inayoashiria ustawi wa kiwango kikubwa ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.
-
Miradi ya nyuklia ya Iran inaweza kuangamizwa?
Apr 12, 2025 13:11Kuna swali jepesi linaloulizwa lakini muhimu; nalo ni: kwa nini mpango wa nyuklia wa Iran hauwezi kuangamizwa, tena hata kwa shambulio la kijeshi?
-
Iran: Tunataka makubaliano ya haki, heshima na usawa; Israel yaingiwa na kiwewe
Apr 12, 2025 08:50Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu inataka makubaliano ya haki na ya heshima, na yaliyojadiliwa kwenye mazingira ya usawa. Sayyid Araghchi amesema hayo kabla ya kuanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na wawakilishi wa Marekani.