-
IRGC yapokea manowari ya kisasa iliyoundwa na wataalamu wa Iran
Feb 27, 2025 23:15Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimepokea zana na vifaa mbalimbali vya kijeshi vilivyoundwa na kutengenezwa hapa nchini Iran, ikiwemo meli ya kivita ya Shahidi Rais Ali Delvari na makumi ya meli za mashambulizi ya haraka zenye mifumo ya kurusha makombora.
-
Iran na Malaysia zasisitiza kuimarisha zaidi ushirikiano
Feb 27, 2025 23:14Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Malaysia wamesisitiza azma ya nchi zao ya kuimarisha Zaidi uhusiano na ushirikiano katika mbalimbali.
-
Baqaei: Kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha uvunjaji sheria wa Israel nchini Syria
Feb 27, 2025 08:17Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha uvunjaji sheria wa utawala haramu wa Israel nchini Syria
-
Rais wa Iran ataka kuimarishwa uhusiano wa mataifa ya Waislamu
Feb 27, 2025 07:33Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amesema kuimarisha maelewano na uhusiano miongoni mwa nchi za Kiislamu zikiwemo Iran na Malaysia ni miongoni mwa mambo ya lazima katika hali ya sasa ya kimataifa.
-
Iran yasambaratisha mtandao wa magaidi wakufurishaji na kunasa silaha nyingi
Feb 27, 2025 04:34Katika operesheni kubwa ya kupambana na ugaidi, vikosi vya usalama vya Iran vimesambaratisha mtandao mkubwa wa magaidi wakufurishaji na kukamata silaha na mabomu kadhaa katika mkoa wa kusini-mashariki wa Sistan na Baluchestan.
-
Msikiti wa Mosalla Tehran kupanuliwa kuwa msikiti mkubwa zaidi duniani
Feb 27, 2025 04:27Eneo kubwa la Swala la Tehran maarufu kama Mosalla Imam Khomeini litapanuliwa na kuwa msikiti mkubwa zaidi duniani.
-
Mkuu wa IRGC: Maadui wa Iran bado hawajapata vipigo 'vikali'
Feb 26, 2025 10:07Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amepongeza uwezo wa kiulinzi na kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, maadui wa Iran bado hawajapata vipigo 'vikali' licha ya mashambulizi na operesheni kadhaa za kulipiza kisasi zilizofanywa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
-
Iran yataka kuwepo uadilifu, kuheshimiana na amani ya kimataifa
Feb 26, 2025 03:11Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva amesisitiza dhamira ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuunga mkono ulimwengu wa pande kadhaa, sheria za kimataifa na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kutoa wito wa kuwepo ulimwengu unaozingatia uadilifu, heshima na amani.
-
Pezeshkian: Iran imeazimia kuimarisha ushirikiano na Russia
Feb 25, 2025 23:17Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian ameahidi kunyanyua kiwango cha uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu na Russia kwa kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya pande mbili, na kuimarisha maingiliano athirifu katika masuala ya kikanda.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran awaonya maadui kuhusu 'jibu kali'
Feb 25, 2025 22:52Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa vijana wa Jamhuri ya Kiislamu kwa hakika wako tayari kutoa "jibu kali na la kusikitisha" kwa kosa lolote la maadui wao, huku akiwaenzi vijana kujitolea kwao katika kulinda usalama wa taifa.