-
Waziri wa Ulinzi wa Iran awaonya maadui kuhusu 'jibu kali'
Feb 25, 2025 22:52Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa vijana wa Jamhuri ya Kiislamu kwa hakika wako tayari kutoa "jibu kali na la kusikitisha" kwa kosa lolote la maadui wao, huku akiwaenzi vijana kujitolea kwao katika kulinda usalama wa taifa.
-
Araghchi: Iran haitafanya mazungumzo na Marekani maadamu mashinikizo yapo
Feb 25, 2025 22:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, katika mkutano wa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, mjini Tehran, amesea hakuna mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yatakayofanyika maadamu Washington inaendeleza sera sera 'Mashinikizo ya Juu Zaidi' dhidi ya Iran.
-
Spika Qalibaf: Namna Hizbullah ilivyoonyesha nguvu zake imedhihirika kuwa Muqawama hauondosheki
Feb 25, 2025 07:09Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, kutokana na jinsi Hizbullah ilivyoonyesha nguvu na uwezo wake, imemdhihirikia wazi kila mtu kwamba maadui hawawezi kuuondoa Muqawama au kuuweka kando ya ulingo wa kisiasa na kiusalama wa Lebanon kutokana na uungaji mkono wa wananchi ilionao.
-
Kuendelea kupiga kambi kwa nguvu na satua msafara wa Manowari za Jeshi la Wanamaji la Iran katika maji ya kimataifa
Feb 25, 2025 00:34Admirali Shahram Irani, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa Msafara wa Manowari Nambari 5 za jeshi hilo umepiga kambi katika eneo la maji ya kimataifa.
-
Araqchi: Silaha za nyuklia za Israel ni tishio na hatari kwa dunia
Feb 24, 2025 23:01Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa jamii ya kimataifa inapasa kuushinikiza utawala wa Israel kujiunga na Mkataba Unaozuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) ili shughuli zake za nyuklia ziwe chini ya usimamizi na ukaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA).
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Sayyed Nasrullah ni kielelezo cha ushujaa na muqawama
Feb 24, 2025 03:45Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Aziz Nasirzadeh, amesema kuwa, Katibu Mkuu wa Hizbullah, Shahidi Sayyed Hassan Nasrullah, alionyesha kielelezo cha kuigwa cha ushujaa na imani katika njia ya muqawama ambayo aliifuata.
-
Spika wa Bunge la Iran: Trump anataka kuwahamisha watu wa Gaza na kupora ardhi ya Palestina
Feb 24, 2025 03:44Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mpango wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kutaka kuwahamisha kwa nguvu watu wa Gaza na kupora ardhi ya Palestina na kubainisha kwamba, mpango huo katu haukubaliki.
-
Je, unaujua mtazamo wa Iran kuhusu uhusiano na nchi za Afrika?
Feb 23, 2025 23:39Mohammad Reza Aref, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao na wakuu wa balozi za nchi za Afrika zilizopo mjini Tehran kwamba: Kukuza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na bara la Afrika ni moja ya vipaumbele vya siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Muqawama wa kukabiliana na ughasibu, dhulma na uistikbari si wa kumalizika
Feb 23, 2025 09:50Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu na ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kufanyika mazishi na maziko ya Mwanajihadi mkubwa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Shahidi Sayyid Hashim Safiyyuddin na kusisitiza kuwa: "adui ajue kwamba, Muqawama wa kukabiliana na ughasibu, dhulma na uistikbari si wa kumalizika; na kwa idhini ya Allah utaendelea hadi ufikie lengo ulilokusudia".
-
Pezeshkian: Mashahidi Nasrullah na Safiyuddin walibakia watiifu kwa viapo vyao hadi mwisho
Feb 23, 2025 04:37Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaenzi na kuwakumbuka kwa wema Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyuddin wakati huu ambapo shughuli ya mazishi ya nguzo hizo mbili kubwa za kambi ya Muqawama ikiendelea.