-
Iran: Iwapo usalama wetu utahatarishwa, mchokozi hatobaki salama
Feb 20, 2025 22:57Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema: Iwapo usalama wa taifa letu utahatarishwa, basi usalama wa eneo hili zima la Kusini Magharibi mwa Asia, wahusika wa uchokozi huo na waungaji mkono wao utavurugwa na hawatobaki salama.
-
IAEA: Tumekubaliana na Iran tuendeleze falsafa ya mapatano ya JCPOA
Feb 20, 2025 22:56Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesema katika mazungumzo na waandishi wa habari mjini Tokyo Japan kuwa: "Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwamba "falsafa ya JCPOA" ambayo msingi wake ni "kuchukua Iran hatua za hiari mkabala wa kupewa upendeleo na motisha," inaweza kuendelea.
-
Mwanadiplomasia wa Iran: Marekani, Israel zinajua vyema uwezo halisi wa Iran
Feb 20, 2025 07:54Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisiasa, Majid Takht Ravanchi amesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zitalazimika kulipa gharama kubwa iwapo zitafanya makosa yoyote dhidi ya Iran.
-
Kwa nini Iran inakaribisha kuimarisha na kupanua uhusiano na nchi jirani?
Feb 20, 2025 07:02Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Russia, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, Waziri Mkuu wa Tajikistan na Naibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Turkmenistan. Mazungumzo haya yamefanyika pambizoni mwa Mkutano wa Tatu wa Kiuchumi wa Eneo la Kaspi hapa mjini Tehran.
-
Spika wa Bunge la Iran: Jinai za Israel Gaza na Lebanon ni mauaji ya kimbari
Feb 20, 2025 04:12Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, jinai za utawala ghasibu wa Israel Gaza na Lebanon ni mauaji ya kimbari.
-
Ziyad al-Nakhala: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni egemeo la makundi ya muqawama
Feb 20, 2025 04:11Ziyad Al-Nakhala, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad al-Islami ya Palestina amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni egemeo na muungaji mkono wa makundi ya muqawama.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Kupanua uhusiano na majirani ni sera ya uhakika ya Iran
Feb 19, 2025 23:36Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: kupanua uhusiano na majirani ni sera ya uhakika ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
IRGC ya Iran yavunja mitandao ya ujasusi ya Israel na Marekani
Feb 19, 2025 23:13Vikosi vya kiintelijensia vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) vimesambaratisha mitandao kadhaa ya kijasusi yenye mfungamano na Marekani na Israel katika mkoa wa Mazandaran, kaskazini mwa nchi.
-
Rais Pezeshkian: Iran, Qatar zinafungua njia mpya za ushirikiano
Feb 19, 2025 12:04Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema Tehran na Doha zimefanya maamuzi muhimu ili kuimarisha uhusiano na kufungua njia mpya za ushirikiano.
-
Abbas Araghchi na Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi walijadili mambo gani?
Feb 19, 2025 08:57Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbusha kuhusu uungaji mkono ulioonyeshwa na nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa hatua ya maana iliyochukuliwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ya kukabiliana na mpango wa pamoja wa Marekani na utawala wa Kizayuni unaolenga kuifuta Palestina, na akabainisha kwamba: "Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuiunga mkono Palestina kwa msimamo thabiti."