-
Rais Pezeshkian: Mazungumzo ya Iran na Marekani ni ‘fursa nzuri’ ya kutatua suala la nyuklia
Feb 09, 2026 22:57Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran yanatoa fursa nzuri ya kufikia suluhu “inayoridhisha pande zote ” kuhusu suala la nyuklia la Iran.
-
Kiongozi Muadhamu awataka Wairani kuwakatisha tamaa maadui Bahman 22
Feb 09, 2026 07:20Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa wito kwa taifa la Iran kuonyesha irada, azma thabiti na kusimama kidete, kwa kushiriki kwa wingi katika matembezi na mijumuiko ya kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu, akisema kuwa umoja huo utamkatisha tamaa adui wa nchi hii.
-
Spika: Iran inajiimarisha kijeshi sambamba na diplomasia
Feb 09, 2026 06:41Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad-Bagher Ghalibaf amesema Jamhuri ya Kiislamu inafuatilia diplomasia sanjari na kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi na kijeshi ili iweze kukabiliana na maadui zake.
-
Jeshi la Iran: Vidole vyetu viko kwenye kitufe cha kufyatua risasi, lakini hatutaki kuanzisha vita
Feb 09, 2026 03:25Mkuu wa vikosi vya Ulinzi vya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, na Kamanda wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, wamesisitiza kuwa, Iran haitafuti kuanzisha vita vya kikanda licha ya utayari wake kamili.
-
Pezeshkian: Iran haikubali mabavu na mantiki yake ya nyuklia imejikita katika Mkataba wa NPT
Feb 08, 2026 23:31Rais Masoud Pezeshkian amepongeza duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani na kuitaja kuwa “hatua ya kusonga mbele,” akisisitiza kuwa msimamo wa Tehran kuhusu suala hilo unategemea haki zilizoainishwa ndani ya Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).
-
Jenerali Mousavi: Iran iko tayari kikamilifu kutoa jibu la haraka na kali kwa uchokozi wowote
Feb 08, 2026 23:30Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa ingawa Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kikamilifu kutoa jibu la haraka, kali na litakaloleta majuto kwa uchokozi wowote, haina nia ya kuanzisha vita vya kikanda.
-
Uwezo wa kiuchumi wa Iran wa kushiriki katika masoko yanayoinukia
Feb 08, 2026 05:53Waziri wa Masuala ya Uchumi na Fedha wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa pili wa masoko yanayoinukia.
-
Iran kuokoa dola milioni 30 kwa kujizalishia aina 63 za dawa
Feb 08, 2026 05:44Iran imezindua bidhaa mpya 63 za dawa zinazozalishwa ndani ya nchi—ikiwa ni pamoja na fomula 19 zinazozalishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini—hatua inayotarajiwa kuifanya nchi hiyi iokoe kati ya dola milioni 25 na 30 kila mwaka kwa fedha muhimu za kigeni, kwa kupunguza utegemezi wa dawa na malighafi zinazoagizwa kutoka nje.
-
Araqchi: Iran haiogopi kutumwa wanajeshi wa upande mwingine katika kanda hii
Feb 08, 2026 05:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu haiogopi vitisho vya kijeshi, akisema: "Iran ni nchi nchi inayofuata diplomasia na mantiki, na wakati huo huo iko tayari kujilinda ili upande wowote usithubutu kulazimisha vita dhidi ya taifa la Iran."
-
Iran yasisitiza kuwa itavishambulia vituo vya kijeshi vya Marekani, si ardhi za nchi jirani
Feb 08, 2026 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ameonya kwamba, iwapo Marekani itaishambulia Iran, vituo vya kijeshi vya nchi hiyo katika eneo la Asia Magharibi navyo vitashambuliwa.