-
Araghchi aziandikia barua nchi jirani: Tutatoa jibu kali mno kwa uchokozi wowote dhidi ya Iran
Dec 31, 2025 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewaandikia barua mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa nchi jirani na kutaka kulaaniwa waziwazi na kwa uthabiti; bwabwaja na upayukaji wa Trump na Netanyahu akitangaza kwamba, Iran haitosita kutoa jibu kali na la kumjutisha yeyote atakayeshiriki kwenye uchokozi dhidi yake.
-
Dey 9, nembo ya mshikamano wa kitaifa mbele ya njama za maadui wa Iran
Dec 31, 2025 02:46Jana Jumanne, kona zote za Iran ya Kiislamu zilishuhudia maandamano makubwa ya wananchi ya kuadhimisha siku inayojulikana kwa jina la Dey 9 ambapo tarehe kama hiyo mwaka 1388 Hijria Shamsia (Disemba 30, 2009) mamilioni ya wananchi wa Iran walimiminika mitaani kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusambaratisha fitna kubwa ya adui.
-
Iran yajibu mapigo, yalitambua jeshi la majini la Canada kama shirika la kigaidi
Dec 30, 2025 23:29Iran imetangaza kulitambua Jeshi la Wanamaji la Canada kama shirika la kigaidi, ikijibu uamuzi wa huko nyuma wa Ottawa wa kuliorodhesha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kama kundi la kigaidi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilisema hayo jana Jumanne.
-
Velayati: Maadui walikosea sana kutweza nguvu za kijeshi za Iran
Dec 30, 2025 23:00Katibu Mkuu wa Majlisi ya Uamsho ya Kiislamu Duniani amesema kuwa, maadui wa Iran walikosea sana katika mahesabu yao juu ya nguvu za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu, kwani makombora yenye usahihi mkubwa ya Iran yalipenya safu nyingi za mifumo ya ulinzi na kupiga kwa usahihi shabaha zilizokusudiwa, na kubadilisha kikamilifu mlingano wa nguvu katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Majeshi ya Iran: Tumejiandaa kutoa pigo kali kwa uchokozi wowote wa adui
Dec 30, 2025 07:15Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimetangaza kuwa, vimejiandaa kikamilifu kutoa majibu makali kwa tishio lolote la usalama wa Jamhuri ya Kiislamu na watu wake na kuonya kwamba, uchokozi wowote mpya wa uadui dhidi ya Iran utakuwa mkali zaidi, angamizi zaidi na wenye madhara makubwa zaidi kuliko huko nyuma.
-
Iran yaonya: Israel inalenga kudhoofisha uthabiti kwa kutambua 'Somaliland' kama nchi huru
Dec 30, 2025 03:07Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga kwa mara nyingine hatua ya utawala wa Kizayuni kutangaza kutambua eneo la Somaliland la Somalia kama nchi huru, ikieleza kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kuleta machafuko katika eneo.
-
Iran yajibu vitisho vya Trump, yaapa kwamba 'jibu kali' litatolewa kwa uchokozi wowote
Dec 29, 2025 23:56Admirali Ali Shamkhani, Mshauri mwandamizi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelaani vikali vitisho vipya vilivyotolewa na Marekani vya kuishambulia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu, akiapa kuwa jibu kali litatolewa endapo utafanywa uchokozi wowote ule.
-
Araqchi: Jenerali Soleimani alikuwa 'Mbunifu wa Mhimili wa Muqawama' Magharibi mwa Asia
Dec 29, 2025 08:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemsifu shahidi na kamanda wa vita dhidi ya ugaidi, Luteni Jenerali Qassim Soleimani na kumtaja kuwa "mbunifu wa Mhimili wa Muqawama" katika eneo Magharibi mwa Asia.
-
Jeshi la Iran: Tupo katika hali bora zaidi kumkabili adui
Dec 29, 2025 06:23Jeshi la Iran limeonya kwamba, hatua yoyote ya uadui kutoka kwa maadui itakabiliwa na jibu kali, huku likisisitiza juu ya utayarifu wake wa kulilinda na kulihami taifa.
-
Araqchi: Tunaunga mkono mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya Yemen
Dec 29, 2025 04:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi amesema kuna ulazima wa kulindwa umoja wa ardhi na mamlaka ya kujitawala ya Yemen, huku kukiwa na ongezeko la mvutano katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.