-
Araghchi aziandikia barua nchi jirani: Tutatoa jibu kali mno kwa uchokozi wowote dhidi ya Iran
Dec 31, 2025 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewaandikia barua mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa nchi jirani na kutaka kulaaniwa waziwazi na kwa uthabiti; bwabwaja na upayukaji wa Trump na Netanyahu akitangaza kwamba, Iran haitosita kutoa jibu kali na la kumjutisha yeyote atakayeshiriki kwenye uchokozi dhidi yake.
-
Imarati yajiondoa kijeshi baada ya ndege za Saudia kushambulia mamluki wake Yemen
Dec 31, 2025 02:49Wizara ya Ulinzi ya Imarati imetangaza kwamba imeamua kujiondoa kijeshi nchini Yemen baada ya ndege za kivita za Saudia kushambulia mamluki wa Imarati kwenye bandani ya Mukalla ya Yemen.
-
2025, mwaka ulioangamiza wanajeshi wengi zaidi wa Israel
Dec 31, 2025 02:48Jeshi la Israel limetoa takwimu kuhusu kuangamizwa idadi kubwa zaidi ya wanajeshi wake mwaka huu wa 2025 unaoisha leo Jumatano na kutangaza kwamba 14% ya maangamizi hayo yametokana na vifo vya kujiua.
-
Rais wa Somalia akutana na rais mwenzake wa Uturuki, wazungumzia Somaliland
Dec 31, 2025 02:47Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amekutana na kufanya mazungumzo na Rais mwenzake wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud mjini Istanbul na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo kadhia ya Somaliland.
-
Dey 9, nembo ya mshikamano wa kitaifa mbele ya njama za maadui wa Iran
Dec 31, 2025 02:46Jana Jumanne, kona zote za Iran ya Kiislamu zilishuhudia maandamano makubwa ya wananchi ya kuadhimisha siku inayojulikana kwa jina la Dey 9 ambapo tarehe kama hiyo mwaka 1388 Hijria Shamsia (Disemba 30, 2009) mamilioni ya wananchi wa Iran walimiminika mitaani kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusambaratisha fitna kubwa ya adui.
-
Iran yajibu mapigo, yalitambua jeshi la majini la Canada kama shirika la kigaidi
Dec 30, 2025 23:29Iran imetangaza kulitambua Jeshi la Wanamaji la Canada kama shirika la kigaidi, ikijibu uamuzi wa huko nyuma wa Ottawa wa kuliorodhesha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kama kundi la kigaidi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilisema hayo jana Jumanne.
-
Kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Mamadi Doumbouya, ashinda urais kwa kishindo
Dec 30, 2025 23:28Tume ya uchaguzi ya Guinea Conakry ilitangaza jioni ya jana Jumanne kwamba kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, Mamadi Doumbouya, ameshinda kwa kishindo kwa kupata asilimia 86.72 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais.
-
Velayati: Maadui walikosea sana kutweza nguvu za kijeshi za Iran
Dec 30, 2025 23:00Katibu Mkuu wa Majlisi ya Uamsho ya Kiislamu Duniani amesema kuwa, maadui wa Iran walikosea sana katika mahesabu yao juu ya nguvu za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu, kwani makombora yenye usahihi mkubwa ya Iran yalipenya safu nyingi za mifumo ya ulinzi na kupiga kwa usahihi shabaha zilizokusudiwa, na kubadilisha kikamilifu mlingano wa nguvu katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Araghchi: Wananchi wa Venezuela watalinda uhuru wao mkabala wa uhalifu wa US
Dec 30, 2025 22:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesisitiza upinzani wa moja kwa moja wa Tehran dhidi ya hatua yoyote ya vitisho dhidi ya ardhi, uhuru na mamlaka ya kujitawala Venezuela, akisisitiza kuwa ana imani kuwa taifa hilo la Amerika Kusini litalinda uhuru wake.
-
Maandamano ya kuilaani Israel kwa 'kuitambua Somaliland' yaenea kote Somalia
Dec 30, 2025 22:56Maelfu ya wananchi wa Somalia wameendelea kumiminika mabarabarani katika miji mbali mbali ya nchi hiyo, kupinga na kulaani uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kulitambua eneo la Somaliland la kaskazini mwa nchi kama taifa huru.