-
Iran yaonya: Israel inalenga kudhoofisha uthabiti kwa kutambua 'Somaliland' kama nchi huru
Dec 30, 2025 03:07Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga kwa mara nyingine hatua ya utawala wa Kizayuni kutangaza kutambua eneo la Somaliland la Somalia kama nchi huru, ikieleza kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kuleta machafuko katika eneo.
-
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakemea Israel kwa kutambua 'Somaliland'
Dec 30, 2025 03:05Wengi wa wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekemea hatua ya utawala wa Israel ya kutambua eneo la Somalia la Somaliland kama nchi huru. Baadhi ya mataifa yameeleza wasiwasi kuwa hatua hiyo inaweza kuathiri kwa kiwango kikubwa hali ya Wapalestina huko Gaza.
-
Khaleda Zia, Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Bangladesh, afariki dunia akiwa na miaka 80
Dec 30, 2025 03:04Begum Khaleda Zia, aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Bangladesh na kiongozi mashuhuri katika siasa za taifa hilo, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 80.
-
Misri yaitisha kikao cha dharura cha Umoja wa Afrika kupinga hatua ya Israel kutambua "Somaliland"
Dec 30, 2025 03:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty, Jumatatu alitoa wito wa kufanyika kikao cha dharura cha Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ili kupinga hatua ya utawala wa Israel kutambua jimbo lililojitenga na Somalia la Somaliland kama nchi huru.
-
Iran yajibu vitisho vya Trump, yaapa kwamba 'jibu kali' litatolewa kwa uchokozi wowote
Dec 29, 2025 23:56Admirali Ali Shamkhani, Mshauri mwandamizi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelaani vikali vitisho vipya vilivyotolewa na Marekani vya kuishambulia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu, akiapa kuwa jibu kali litatolewa endapo utafanywa uchokozi wowote ule.
-
Mahabusu 100 wa Kipalestina wameuawa katika jela za Israel ndani ya miaka miwili
Dec 29, 2025 23:15Wataalamu wa Palestina wamefichua ukatili na ukandamizaji unaowakabili mahabusu na mateka wa Palestina katika magereza ya utawala wa Israel na mienendo isiyo ya kibinadamu na ukatili wa Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala huo dhidi ya wafungwa wa Kipalestina.
-
Ripoti: Hasara ya majanga ya hali ya hewa mwaka 2025 imezidi dola bilioni 120
Dec 29, 2025 23:15Ripoti mpya inaonyesha kwamba mawimbi ya joto yaliyovunja rekodi, vimbunga vya kitropiki na mvua zilizosababisha mafuriko makubwa kote duniani, vimeufanya mwaka unaomalizika wa 2025 kuwa moja ya miaka yenye hasara kubwa zaidi kwa majanga ya hali ya hewa, huku hasara za kiuchumi zikikadiriwa kuwa karibu dola bilioni 120.
-
Chuo Kikuu cha Georgetown, US chamfukuza Ripota wa UN aliyeanika jinai za Gaza
Dec 29, 2025 23:15Francesca Albanese, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu amesema hatua ya Chuo Kikuu cha Georgetown cha Marekani ya kukata uhusiano naye ni sehemu ya vikwazo alivyowekewa na Washington kwa kufichua mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza, na ushiriki wa Marekani katika jinai hizo.
-
Makumbusho ya taifa ya Libya yafunguliwa tena baada ya miaka 14
Dec 29, 2025 23:14Kufunguliwa tena kwa Jumba la Makumbusho Taifa la Libya baada ya kufungwa kwa miaka 14 kunatoa matumaini ya kurejea utulivu nchini humo na kujumuishwa utambulisho wa kitaifa.
-
Ni kwa sababu gani Katibu Mkuu wa NATO anang'ang'ania Ulaya iendelee kuwa tegemezi kiulinzi kwa Marekani?
Dec 29, 2025 23:14Katibu Mkuu wa shirika la kijeshi la NATO, Mark Rutte ameshikilia msimamo wa kutaka nchi za Ulaya ziendelee kuwa tegemezi kiulinzi kwa Marekani.