-
UN: Zaidi ya watu 10,000 wamelazimika kuhama makwao ndani ya siku tatu nchini Sudan
Dec 29, 2025 03:02Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa zaidi ya watu 10,000 wamelazimika kuhama makazi yao katika siku tatu katika majimbo ya Darfur Kaskazini na Kordofan Kusini mwa Sudan, huku vita vikiendelea nchini humo kati ya jeshi la taifa na wanamgambo wa RSF.
-
Kanali Msaudia: Imarati inafanya njama za kuigawa vipande vipande Saudi Arabia + Video
Dec 29, 2025 02:53Kanali mmoja mstaafu wa jeshi la Saudia ametoa kauli kali ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) akisema kuwa, nchi hiyo ni mkono wa utawala wa Kizayuni unaofanya kazi ya kuzidhoofisha na kuziangamiza nchi za Kiarabu na hasa Saudi Arabia.
-
Mawimbi ya kwanza ya satelaiti tatu za Iran yapokewa ardhini kwa mafanikio + VIDEO
Dec 28, 2025 23:51Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran ametangaza kwamba mawimbi ya kwanza ya satelaiti zote tatu zilizobuniwa na kutengenezwa ndani ya Iran zinazoitwa "Zafar 2", "Paya" na "Kowsar" zilizotumwa angani Jumapili jioni Disemba 28, 2025 yamepokewa kwa mafanikio ardhini akisisitiza kuwa, hii inathibitisha uzima wa kiufundi na utendajikazi mzuri wa satelaiti hizo za Iran baada ya kuingia kwenye obiti.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Kuupokonya silaha Muqawama ni mradi wa kuangamiza nguvu za Lebanon
Dec 28, 2025 23:51Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon ya Hizbullah amesema: "leo, Lebanon iko katikati ya dhoruba na mvurugiko wa utulivu kutokana na sera za Marekani na adui wa Kizayuni."
-
Uchaguzi wa urais Kenya ukifanyika leo Ruto atashinda, lakini utaingia katika duru ya pili
Dec 28, 2025 23:50Utafiti uliofanywa na kampuni ya Infotrak unaonyesha kuwa, endapo uchaguzi wa urais wa Kenya ungefanyika hivi leo, Rais William Ruto angeibuka mshindi; hata hivyo uchaguzi huo ungelazimu kuingia katika duru ya pili kwa sababu ushindi wake usingevuka kiwango cha asilimia 50+1 ya kura kinachohitajika.
-
Vikwazo vya UK vyazilazimisha Angola na Namibia zikubali kupokea wahamiaji wanaorejeshwa
Dec 28, 2025 23:50Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza imetangaza kuwa, Angola na Namibia zimekubali kuruhusu kurejeshwa katika nchi hizo wahamiaji wasio rasmi na wahalifu baada ya serikali ya Uingereza kutishia kutoa adhabu ya vikwazo vya viza kwa nchi zinazokataa kutoa ushirikiano.
-
Korea Kusini yalazimika kufunga skuli 4,000 kwa kukosekana wanafunzi
Dec 28, 2025 23:49Wizara ya Elimu ya Korea Kusini imetangaza kuwa, skuli 4,008 za msingi, za kati na sekondari zimefungwa kote nchini humo kutokana na kupungua kwa kasi idadi ya wanafunzi, huku mamia ya taasisi za elimu na mafunzo zikibaki bila ya matumizi.
-
China yaikosoa sera ya Marekani ya kulinda ubabe wake wa kijeshi kwa fitina
Dec 28, 2025 23:05China, katika ukosoaji ulio wazi dhidi ya Marekani, imetangaza kuwa Washington, kwa ajili ya kulinda ubabe wake wa kijeshi, inajihusisha na mbinu za kutia fitna, kugawa na kutawala.
-
Satelaiti tatu za Iran zarushwa katika anga za mbali, ni hatua madhubuti ya kiteknolojia
Dec 28, 2025 09:31Satelaiti tatu za Iran zilizoundwa ndani ya nchi , ‘Paya’, ‘Zafar 2’ na ‘Kowsar’, leo zimerushwa katika anga za mbali kwa kutumia roketi ya kubeba satelaiti aina ya Soyuz kutoka kituo cha anga cha Vostochny kilichoko nchini Russia.
-
Baraza la Usalama na Arab League kukutana kujadili hatua ya Israel ya kuitambua rasmi Somaliland
Dec 28, 2025 08:07Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) zimepanga kufanya mikutano tofauti wiki hii kujadili matokeo ya hatua ya Israel ya kulitambua rasmi eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.