-
Wanawake na watoto ni kati watu zaidi ya 200 waliouawa katika mauaji mapya ya kikabila huko Darfur
Dec 28, 2025 07:09Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa watu zaidi ya 200, wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika mashambulizi ya kikabila yaliyofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur nchini Sudan.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Qatar wajadili matukio ya kikanda hasa hali ya Yemen
Dec 28, 2025 06:59Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Qatar wamezungumza kwa njia ya simu na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya kikanda hususan matukio ya karibuni huko Yemene. Wamesema kuwa ipo haja ya kulindwa mamlaka ya kujitawal ya ardhi nzima ya nchi hiyo.
-
Putin: Russia itatumia nguvu za jeshi iwapo Ukraine itakwamisha mazungumzo ya amani
Dec 28, 2025 06:58Rais wa Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa Moscow iko tayari kutumia nguvu za kijeshi kufikia malengo ya operesheni yake maalumu ya kijeshi iwapo Ukraine itaendelea kuchelewesha mazungumzo ya amani.
-
Jamhuri ya Afrika ya Kati yaendesha uchaguzi mkuu,Touadéra anawania muhula wa tatu wa urais
Dec 28, 2025 06:52Raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wameelekea kwenye masanduku ya kura katika zoezi la uchaguzi mkuu huku Rais Archange Touadéra akiwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
-
Iran: Tumejiandaa kutoa jibu chungu zaidi kwa wavamizi
Dec 28, 2025 03:17Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameonya kwamba, kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kitakabiliwa na jibu la haraka na la kuumiza zaidi, akisisitiza utayarifu wa Vikosi vya Jeshi vya nchi hii kukabiliana na maadui na vitisho vyao.
-
Balozi wa Iran nchini Russia na Mufti wa Moscow wasisitiza ushirikiano wa kidini
Dec 28, 2025 03:16Kazem Jalali, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Russia amekutana na kufanya mazungumzo na Albir Hazrat Krganov, Mufti wa Moscow na Mwenyekiti wa Baraza la Kiroho la Waislamu wa Russia, na kujadili namna ya kupanua ushirikiano wa kidini.
-
Dunia yaendelea kulaani hatua ya Israel ya 'kuigawa vipande' Somalia
Dec 28, 2025 03:15Nchi za dunia na taasisi mbali mbali za kimataifa zimeendelea kulaani uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kutambua eneo la Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
-
Russia yasisitiza haja ya kuundwa taifa huru la Palestina
Dec 28, 2025 03:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amesema kwamba, Moscow ingali inaunga mkono suuala la kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.
-
WHO: Unywaji wa pombe unaua watu 800,000 kila mwaka Ulaya
Dec 28, 2025 03:05Unywaji wa pombe unasababisha vifo vya watu zaidi ya 800,000 kila mwaka barani Ulaya, na kusababisha kifo kimoja kati ya kila vifo kumi na moja, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO).
-
Iran yalaani shambulio la kigaidi katika msikiti wa Imam Ali (as) nchini Syria
Dec 28, 2025 00:14Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani shambulio la kigaidi dhidi ya waumini katika Msikiti wa Imam Ali ibn Abi Talib (AS) katika kitongoji cha Wadi al Dhahab katika mkoa wa Homs , Syria na kuuwa shahidi watu 5 na kujeruhi wengine 21.