-
Nchi 14 zikiwemo za EU zalaani mpango wa ujenzi haramu Ukingo wa Magharibi
Dec 25, 2025 03:10Kundi la nchi 14 zikiwemo za Ulaya limetoa taarifa ya pamoja ya kulaani vikali uamuzi wa Israel wa kuanzisha ujenzi mpya wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu, na kuitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
-
40 wauawa, kujeruhiwa katika shambulio la bomu Msikitini Maiduguri, Nigeria
Dec 25, 2025 02:13Mripuko mkubwa wa bomu umeripotiwa kutikisa Msikiti mmoja wakati wa Swala ya Magharibi usiku wa kuamkia leo huko mjini Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
UWW: Muirani Amouzad ndiye mwanamieleka 'Aliyetamalaki Zaidi' duniani 2025
Dec 25, 2025 02:12Muungano wa Mieleka Duniani (UWW) umemtaja Rahman Amouzad kutoka Iran kuwa mwanamieleka wa mtindo wa freestyle (kujiachia) "Aliyeng'ara Zaidi" kwa mwaka huu 2025.
-
Bunge la Algeria laidhinisha sheria inayojinaisha ukoloni wa Ufaransa
Dec 25, 2025 00:03Bunge la Algeria jana Jumatano lilipasisha kwa kauli moja sheria inayotambua ukoloni wa Ufaransa nchini humo kuwa ni jinai, ikiutaja kuwa ni "uhalifu wa serikali," na kuitaka Ufaransa iombe msamaha rasmi kwa jinai hiyo.
-
Iran yasema haikubali ukaguzi wa vituo vya nyuklia vilivyoshambuliwa
Dec 25, 2025 00:02Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki la Iran (AEOI) amesema kuwa shinikizo la kisiasa na kisaikolojia kuhusu ukaguzi wa vituo vya nyuklia vilivyoharibiwa katika mashambulizi ya Israel na Marekani halitakuwa na athari yoyote, akisisitiza haja ya kuwepo taratibu zilizo wazi kwa hali kama hizo.
-
Wapiganaji wawateka wasafiri Waislamu nchini Nigeria
Dec 24, 2025 23:16Watu wenye silaha wamewateka nyara wasafiri 28 Waislamu katikati ya Nigeria, mamlaka zimeripoti, likiwa ni tukio jipya katika wimbi la utekaji nyara linalotikisa taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.
-
Hamas yasisitiza kuwa haitaweka chini silaha
Dec 24, 2025 23:09Harakati ya Kiislamu (Muqawama) ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, Hamas, imetangaza wazi kuwa haitakubali jaribio lolote la kuipokonya silaha, ikionya dhidi ya kuingiliwa mambo ya Palestina na mataifa ya kigeni. Hamas imesisitiza kuwa inahitaji dhamana zilizo wazi na madhubuti zaidi kwa awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano na utawala wa Israel.
-
UN yaongeza muda wa kuhudumu askari AUSSOM nchini Somalia
Dec 24, 2025 23:08Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuongeza muda wa Ujumbe wa Umoja wa Afrika wa Msaada na Kurejesha utulivu nchini Somalia (AUSSOM) kwa mwaka mmoja zaidi, hadi tarehe 31 Desemba 2026.
-
Kwa nini Marekani inashadidisha mazingira ya vita dhidi ya Venezuela?
Dec 24, 2025 23:06Marekani, kwa mara nyingine tena, imeimarisha uwepo wake kijeshi huko Caribbean.
-
Pakistan yapinga vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Iran katika faili la nyuklia
Dec 24, 2025 09:50Mwakilishi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amepinga vikali vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Iran katika faili la nyuklia.