-
Raia 104 wameuawa katika mashambulizi ya droni Kordofan Sudan
Dec 17, 2025 09:13Kwa uchache raia 104 wameuawa katika mashambulizi ya droni, ndege zisizo na rubani katika eneo la Kordofan nchini Sudan tangu Desemba 4 mwaka huu. Hayo yametangazwa na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk na kuelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka vita na mapigano kati ya makundi ya RSF na SAF huko Sudan.
-
Waziri wa Mambo ya Nje asisitizia tena azma ya Iran ya kutetea haki zake za kisheria za nyuklia
Dec 17, 2025 03:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesisitizia azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya kutetea haki zake za kisheria za nyuklia kulingana na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT), akisema sera za nyuklia za Tehran zingali zinaendana na mfumo wa sheria za kimataifa.
-
HAMAS: Israel imekiuka vipengele vyote vya usitishaji vita, makubaliano yako hatarini kuvunjika
Dec 17, 2025 03:09Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ameushutumu utawala wa kizayuni wa Israel kwa ukiukaji mkubwa na uliopangwa wa makubaliano ya kusitisha vita, akionya kwamba kuendelea kwa mwelekeo huo kunayaweka makubaliano hayo katika hatari ya kuvunjika kikamilifu.
-
Waziri Mkuu wa Australia amhutubu Muislamu aliyejitolea maisha yake: Wewe ni shujaa wa Australia
Dec 17, 2025 03:08Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ametembelea Hospitali ya St. George kusini mwa Sydney ili kumjulia hali Ahmed Al Ahmed, Mwislamu aliyehatarisha maisha yake kwa kumvamia na kumpokonya bunduki mmoja wa wahusika wa shambulio lililotokea kwenye Ufukwe wa Bondi na kusababisha vifo vya watu 15.
-
Mke wa rais wa Guinea Bissau aliyepinduliwa akamatwa Ureno kwa tuhuma za kutakatisha pesa
Dec 17, 2025 03:08Mamlaka za nchini Ureno zimemtia nguvuni na kumfungulia mashtaka mke wa rais wa Guinea-Bissau aliyepinduliwa, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusu madai ya utakatishaji fedha. Hayo yameelezwa na polisi ya nchi hyo.
-
Mkuu wa White House akiri: Lengo hasa la kuzishambulia boti ni kumpindua Maduro
Dec 17, 2025 03:07Mkuu wa wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani White House Susie Wiles ametamka kuwa, mashambulizi ya jeshi la Marekani dhidi ya boti zinazodaiwa kuwa ni za madawa ya kulevya yanayofanywa katika eneo la Amerika Kusini yanalenga hatimaye kumpindua Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
-
Qalibaf asisitiza umuhimu wa utafiti katika kutatua matatizo ya kitaifa
Dec 16, 2025 23:21Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa utafiti katika kutatua changamoto na matatizo ya kitaifa.
-
UNICEF: Hali ya maisha kwa watoto Gaza ni majanga
Dec 16, 2025 23:20Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hali ya maisha kwa watoto katika Ukanda wa Gaza ni mbaya mno.
-
Takriban raia 2,000 waukimbia mji wa Heglig, Sudan baada ya kudhibitiwa na kikosi cha RSF
Dec 16, 2025 23:19Duru za habari ndani ya Sudan jana ziliarifu kuwa takriban raia 2,000 wameyaacha makazi yao katika mji wa Heglig wa magharibi mwa Sudan huko Kordofan Magharibi baada ya safari ngumu ya siku tisa ya kuhama makazi yao kufuatia kutekwa mji huo nawanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Tanzania yaendelea kuwa chaguo la watalii wa kimataifa
Dec 16, 2025 23:19Tanzania imeendelea kushuhudia ongezeko la watalii kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya, yakiwemo Ufaransa, wanaovutiwa na uzuri wa kipekee wa asili na mandhari tofauti zinazopatikana katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.