-
Iran: Trump hawezi kuwa mtu wa kuleta amani wakati anachochea vita visivyo na mwisho
Oct 15, 2025 02:33Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amemkosoa vikali Donald Trump kwa sera yake ya kuchochea vita katika eneo la Asia Magharibi, akisema rais wa Marekani hawezi kudai anapigania kuleta amani katika eneo hili huku akifuata sera za uchokozi na kufungamana na "wahalifu wa kivita."
-
Israel yaanza ukhabithi wake, yapunguza misaada ya kuingizwa Ghaza hadi nusu, yazuia fueli kikamilifu
Oct 15, 2025 02:33Utawala wa kizayuni wa Israel umeueleza Umoja wa Mataifa kwamba, kuanzia leo Jumatano utaruhusu malori 300 tu ya misaada kwa siku, ikiwa ni nusu ya idadi iliyokubaliwa kuingia katika Ukanda wa Ghaza na kwamba hakuna mafuta yoyote au gesi itakayoruhusiwa kuingizwa katika eneo hilo isipokuwa kwa mahitaji maalumu yanayohusiana na miundombinu ya kibinadamu.
-
Afrika Kusini: Kesi ya mauaji ya kimbari tuliyofungua ICJ dhidi ya Israel itaendelea licha ya vita kusitishwa
Oct 15, 2025 02:32Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema usitishaji vita wa Ghaza hautaathiri kesi ya mauaji ya kimbari iliyofunguliwa na nchi yake dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
-
Mahakama ya Madagascar "yamwita" kanali wa jeshi akachukue uongozi na kuitisha uchaguzi
Oct 15, 2025 02:32Mahakama ya Juu ya Katiba ya Madagascar jana Jumanne "ilimwita" kamanda wa Kituo cha Uendeshaji cha Wafanyakazi wa Jeshi (CAPSAT) Kanali Michael Randrianirina "akatekeleze kazi za mkuu wa nchi."
-
Chama cha rais wa Gabon chapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Bunge
Oct 15, 2025 02:31Chama tawala cha Rais wa Gabon Brice Oligui Nguema, cha Muungano wa Kidemokrasia wa Wajenzi (Democratic Union of Builders) (UDB) kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Bunge, kwa kunyakua viti 102 kati ya 145 baada ya kutangazwa matokeo ya duru ya kwanza na ya pili ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika nchini humo.
-
Waziri Mkuu wa Uhispania: Usitishaji vita hauipi kinga Israel ya kutoadhibiwa kwa mauaji ya kimbari ya Gaza
Oct 14, 2025 23:55Pedro Sanchez Waziri Mkuu wa Uhispania amesisitiza kuwa makubaliano ya kusitisha vita Gaza yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Israel yasifanywe kuwa fidia ya mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israel Ukanda wa Gaza.
-
Araghchi kuhudhuria mkutano wa NAM nchini Uganda
Oct 14, 2025 23:04Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu, Abbas Araghchi atazuru Uganda karibuni hivi kushiriki Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM).
-
Rajoelina atangaza kulivunja Bunge la Madagascar akiwa 'mafichoni'
Oct 14, 2025 23:04Rais wa Madagascar anayesakamwa na mashinikizo ya kujiuzulu, Andry Rajoelina ametangaza kulivunja Bunge kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali yake kote nchini, akisema ni muhimu kurejesha utulivu na kutoa nafasi kwa vijana.
-
India yaendelea kuwakamata Waislamu wanaosema 'Nampenda Muhammad'
Oct 14, 2025 23:03Watumiaji wa mitandao ya kijamii wameikosoa vikali serikali ya India kwa kuendelea kuwatia mbaroni na kuwashtaki Waislamu wanaoendeleza kampeni ya nchi nzima ya 'Nampenda Muhammad'.
-
Balozi: US inaihangaisha dunia kwa kisingizio cha kuleta 'uhuru'
Oct 14, 2025 23:02Balozi wa Venezuela nchini Iran, José Rafael Silva Aponte amesema Marekani inaihangaisha dunia nzima, ikiwa ni pamoja na Amerika ya Kusini, kwa kutumia kisingizio cha kuleta uhuru katika maeneo tofauti ya dunia, lakini Venezuela daima itasalia kuwa nchi huru na yenye mamlaka ya kujitawala.