-
Kwa nini Trump amekosa Tuzo ya Amani ya Nobel?
Oct 11, 2025 07:37Baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kukosa Tuzo ya Amani ya Nobel, msemaji wa Ikulu ya White House ameikosoa Kamati inayoandaa Tuzo ya Nobel kwa kutomtunuku rais huyo tuzo hiyo, akiitaja hatua hiyo kuwa ni upendeleo wenye kufadhilisha siasa badala ya amani.
-
Wananchi wa Uruguay waandamana wakitaka kukatwa uhusiano na Israel
Oct 11, 2025 05:55Maelfu ya wananchi wa Uruguay waliingia mitaani na mabarabarani jana Ijumaa, kushiriki maandamano ya kuitaka serikali yao itambue mzozo wa kibinadamu unaoendelea Gaza kama mauaji ya halaiki, sanjari na kukata uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi na Israel.
-
Mwandishi wa gazeti la kizayuni la Haaretz: HAMAS haijasambaratika na imefikia malengo yake
Oct 11, 2025 05:39Mwandishi mashuhuri wa gazeti la kizayuni la Haaretz Chaim Levinson amesema, japokuwa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imepoteza hatamu za uongozi wa Ukanda wa Ghaza, lakini imefanikiwa kufikia malengo yake mawili makuu.
-
UNHCR yahimiza kuchukuliwa hatua kukabiliana na tatizo kubwa la wakimbizi katika eneo la Sahel
Oct 11, 2025 04:42Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) jana Ijumaa lilitoa wito wa kutekelezwa juhudi za kimataifa haraka iwezekanavyo ili kukabiliana na mgogoro unaoongezeka wa wakimbizi katika eneo la Sahel barani Afrika, ambapo takriban watu milioni 4 wamelazimika kuhama makazi yao huko Burkina Faso, Mali, Niger na katika nchi nyingine jirani.
-
Chombo cha Kizayuni: Zoezi la kuachiliwa mateka Wapalestina limeanza
Oct 11, 2025 04:34Chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kimetangaza kuwa, zoezi la kuachiliwa huru matekani wa Palestina kutoka jela tano za Israel limeanza.
-
Wazayuni wakiri kushindwa kuivunja na kuipokonya silaha HAMAS
Oct 11, 2025 02:07Duru za habari za utawala wa Kizayuni wa Israel zimekiri kwamba vita vya Ghaza vimeisha na Hamas imepata mafanikio mengi kiasi kwamba licha ya kupita miaka miwili ya mashambulizi ya kila upande lakini Wazayuni wameshindwa kuivunja harakati hiyo kama ambavyo wameshindwa pia kuipokonya silaha.
-
Iran: Tutalinda maslahi yetu Ghuba ya Uajemi hadi tone la mwisho la damu
Oct 11, 2025 02:07Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amegusia uwezekano wa kutokea vita vya moja kwa moja vya kijeshi baina ya Iran na Marekani katika Ghuba ya Uajemi na kusema: Tutajihami na kulinda maslahi yetu katika Ghuba ya Uajemi hadi tone la mwisho la damu.
-
Yemen: Tutaendelea kuitia adabu Israel kama haitoheshimu usimamishaji vita Ghaza
Oct 11, 2025 02:06Mamia ya maelfu ya wananchi wa Yemen walifanya mikutano na maandamano ya nchi nzima kitaifa jana wakielezea kuwa kwao tayari kuendelea kuitandika na kuitia adabu Israel kama haitoheshimu makubaliano ya kusitisha vita na kukomesha jinai zake huko Ghaza.
-
Gen-Z Morocco wamlazimisha mfalme kufanya mageuzi ya kimsingi
Oct 11, 2025 02:06Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco jana Ijumaa alitoa amri ya kufanyika mageuzi ya kimsingi ili kulinda haki za kijamii wakati huu ambapo nchi hiyo imekumbwa na maandamano yanayoongozwa na vijana wanaolalamikia huduma mbovu za kijamii na ukosefu wa usawa.
-
WFP yaonya juu ya kuongezeka njaa miongoni mwa wakimbizi nchini Ethiopia
Oct 11, 2025 02:05Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) jana Ijumaa lilionya kwamba wakimbizi nchini Ethiopia wako katika hatari ya kuteseka zaidi kwa njaa huku uhaba mkubwa wa fedha ukisababisha kupunguzwa mgao wa chakula.