-
Familia 1,200 zahama makazi yao kutokana na mafuriko Khartoum, Sudan
Oct 06, 2025 03:45Zaidi ya familia 1,200 za Sudan zimefurushwa katika nyumba zao na mafuriko katika mji wa Bahri katika jimbo la Khartoum, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilisema hayo jana Jumapili.
-
Kwa nini China inaamini kujitoa Marekani katika JCPOA ndio chanzo cha mgogoro wa sasa kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran?
Oct 06, 2025 02:43China imetangaza kuwa, kujitoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ndio chanzo cha mgogoro unaoshuhudiwa hivi sasa kuhusiana na kadhia ya nyuklia ya Iran.
-
Iran yaunga mkono uamuzi wa Palestina juu ya usitishaji vita Gaza; lakini yaonya...
Oct 06, 2025 02:21Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema itaunga mkono uamuzi wowote wa watu wa Palestina na Muqawama kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano Gaza linaloungwa mkono na Marekani, huku ikiionya jamii ya kimataifa kuhusu mwelekeo hatari wa mpango huo na historia ya kutokuwa na muamana Israel.
-
Timu ya voliboli ya wanawake ya Iran yatwaa ubingwa wa CAVA 2025
Oct 06, 2025 01:49Timu ya voliboli ya wanawake ya Iran iliigaraza Uzbekistan kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji ya Wanawake wa Asia ya Kati (CAVA) jana Jumapili na kushinda taji hilo la kieneo kwa mara ya kwanza katika historia.
-
Waziri Araghchi: Ulaya 'imehafifisha' nafasi yake katika mazungumzo ya siku zijazo ya mpango wa nyuklia wa Iran
Oct 05, 2025 23:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi za Ulaya zimedhoofisha msimamo wao katika mchakato wa kidiplomasia unaolenga kutatua kadhia ya nyuklia ya Iran na kwa hiyo watakuwa nafasi "hafifu" katika mazungumzo yoyote yatakayofanyika siku za usoni.
-
Hizbullah: Mpango wa Trump wa Gaza unalenga 'kuisafisha' Israel
Oct 05, 2025 23:07Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem amekosoa mpango wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu Gaza, na kuutaja kuwa ni hatua hatari ya kuisafisha Israel kutokana na jinai zake na sehemu ya ajenda ya kujitanua utawala huo ghasibu.
-
Bunge la Chad lajiunga na mkondo wa kuondoa ukomo wa mihula ya urais, lamfungulia njia Deby Itno
Oct 05, 2025 22:53Bunge la Chad limeidhinisha kwa wingi mkubwa sana wa kura marekebisho ya katiba yanayoondoa ukomo wa mihula ya urais, na kurefusha muda wa kila muhula kutoka miaka mitano hadi saba, hatua ambayo wakosoaji wanasema ni mbinu ya kuuzatiti utawala wa Rais Mahamat Idriss Deby Itno.
-
Ripoti: Mossad ilihusika katika kutekwa nyara na kuuawa aliyekuwa waziri mkuu wa Italia Aldo Moro
Oct 05, 2025 22:53Ripoti mpya ya uchunguzi iliyotolewa inaonyesha kuwa shirika la ujasusi la utawala wa kizayuni wa Israel, Mossad ilihusika katika kutekwa nyara na kuuawa Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Aldo Moro mwaka 1978, na hivyo kudhihirisha ushawishi mkubwa iliokuwa nao Israel wakati katika uga wa siasa za Italia, ikiwa ni pamoja na kufuatia uhusiano wa Moro na makundi ya Muqawama ya Palestina.
-
Netanyahu ndiye aliyeamuru kushambuliwa kwa droni meli za msafara wa Sumud bandarini Tunisia
Oct 05, 2025 22:52Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa, waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ndiye aliyetoa idhini ya kufanywa mashambulio ya ndege zisizo na rubani yaliyolenga msafara wa kimataifa wa meli za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Ghaza zilizokuwa zimetia nanga kwenye bandari ya Tunisia.
-
Putin aonya: Kuipatia Ukraine makombora ya Tomahawk kutavuruga uhusiano wa Russia na Marekani
Oct 05, 2025 22:52Rais Vladimir Putin wa Russia amesema ikiwa Marekani itaipatia Ukraine makombora aina ya Tomahawk ili kufanyia mashambulio ya masafa marefu ndani ya Russia, hatua hiyo itapelekea kuvurugika husiano wa Moscow na Washington.