-
Rais Ruto: Kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta Afrika Mashariki kujengwa Lamu, Kenya
Jul 11, 2026 04:38Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto, ametangaza hatua kuu ya maendeleo ya kiuchumi Ijumaa hii, akithibitisha kuwa mipango ya ujenzi wa kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta Afrika Mashariki imekamilika.
-
Malalamiko rasmi dhidi ya Infantino wa FIFA kuhusu uhusiano Wake na Trump
Jul 11, 2026 04:32Shirika moja la kutetea haki za binadamu na usimamizi wa michezo limetangaza mpango wake wa kuwasilisha malalamiko dhidi ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino, kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC). Shirika hilo linamtuhumu Infantino kwa kukiuka mara kwa mara sheria za kutofungamana na upande wowote katika masuala ya kisiasa, kupitia uungaji mkono wake wa wazi na uhusiano wa karibu na Rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Wamalawi 38,000 waondoka Afrika Kusini kufuatia maandamano ya ghasia dhidi ya wahamiaji
Jul 11, 2026 03:29Wamalawi 38,000 waondoka Afrika Kusini kufuatia maandamano ghasia dhidi ya wahamiaji
-
'Makubwa zaidi katika historia ya binadamu': Zaidi ya watu milioni 43 wameshiriki mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi nchini Iran, Iraq
Jul 11, 2026 03:09Makumi ya mamilioni ya Wairani na waumini kutoka nchi mbalimbali duniani waligeuza shughuli ya mazishi ya Kiongozi aliyeuawa shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa ajili ya mazishi kote duniani.
-
Mauaji ya kimbari, ubaguzi wa rangi, na ukoloni... Je, Kanisa la Uingereza limeipa mgongo Israel?
Jul 11, 2026 03:03Gazeti la Times la London limeripoti kwamba Rabi Mkuu wa Mayahudi wa Uingereza, Sir Ephraim Mirvis, amelitaka Kanisa la Uingereza kukataa kujadili ripoti inayoelezea vita vya Israel huko Gaza kuwa ni "mauaji ya kimbari," akidai kwamba kupitishwa hati hiyo kunaweza kuharibu uhusiano kati ya Wayahudi na Wakristo uliojengwa kwa miongo kadhaa.
-
Abu Torabifardi: Utaratibu wa makubaliano ni ahadi kwa ahadi
Jul 11, 2026 02:50Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo katika mji wa Tehran amesisitiza kuwa hati ya makubaliano kati ya Iran na Marekani haikuandaliwa kwa msingi wa kuuamini uongozi wa Marekani na kueleza kuwa: Mfumo wa makubaliano hayo ni 'ahadi kwa ahadi'; na tunatangaza wazi wazi kwamba Marekani hataruhusiwa kamwe kuingilia masuala ya Mlango Bahari wa Hormuz.
-
Kamanda mkuu wa Majeshi Iran asema wauaji wa Kiongozi Muadhamu watakabiliwa na adhabu
Jul 11, 2026 02:47Kamanda wa Makao Makuu ya Majeshi ya Iran maarufu kwa jina la Kamandi ya Khatamul-Anbiya (SAW) amesema wale waliohusika na mauaji ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, watakabiliwa na adhabu, akielezea mahudhurio makubwa ya watu katika mazishi yake kuwa ni dhihirisho lenye nguvu la imani, ukakamavu na mshikamano.
-
Wapinzani Kongo wapinga jitihada za Rais Tshisekedi za kuwania muhula wa tatu wa urais
Jul 11, 2026 02:45Wapinzani Kongo wapinga jitihada za Rais Tshisekedi za kuwania muhula wa tatu wa urais
-
Familia nzima imeangamizwa: Amnesty International yaituhumu Israel kufanya uhalifu wa kivita nchini Lebanon
Jul 11, 2026 02:43Shirika la Amnesty International mapema jana Alhamisi lilitoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mashambulizi matatu yaliyofanywa na utawala wa Israel kusini mwa Lebanon mwezi Machi, likiyataja mashambulizi hayo kuwa ni uhalifu wa kivita.
-
Iran: Hatua za Marekani ni mfano wa wazi wa uhalifu mkubwa wa kivita
Jul 11, 2026 02:41Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema, mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya maeneo kadhaa katika mikoa ya pwani ya kusini mwa nchi pamoja na madaraja mawili yaliyopo katika mikoa ya mashariki kwenye njia ya reli inayoelekea mji mtakatifu wa Mashhad, yanajumuisha uhalifu mkubwa wa kivita.