-
Mufti wa Russia: Kiongozi shahidi wa Iran alifanya juhudi kubwa za kuleta umoja wa madhehebu ya Kiislamu
Jul 04, 2026 04:20Mufti na Mwenyekiti wa Baraza la Kidini la Waislamu wa Russia anaamini kuwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kiongozi shahidi wa Iran, wakati wa uhai wake alichukua hatua kubwa katika kuimarisha umoja na maelewano kati ya madhehebu ya Kiislamu.
-
Spika Qalibaf: Kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya Iran na China ni jambo la dharura
Jul 04, 2026 04:15Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kimkakati, kisiasa na kibunge kati ya Tehran na Beijing.
-
Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya janga la haki za binaadamu al-Obeid
Jul 04, 2026 04:12Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk ametahadharisha juu ya janga jingine la haki za binaadamu katika mji wa al-Obeid, nchini Sudan na kuutolea wito ulimwengu kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.
-
Majaribio ya tiba ya Ebola yaanza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Jul 04, 2026 04:09Shirika la Afya Duniani limetangaza kuanza kwa majaribio ya dawa zinazoweza kutibu aina ya virusi vinavyosababisha mlipuko wa sasa wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Iran yaapa kulipiza kisasi kwa Kiongozi Shahidi huku wageni maalum wakimiminika kwa ajili ya mazishi
Jul 03, 2026 11:35Rais wa Iran na Spika wa Bunge wametoa kauli tofauti wakiahidi kuwajibisha tawala katili za Marekani na Israel kwa mauaji ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, huku maafisa wa ngazi za juu kutoka zaidi ya nchi 30 wakikusanyika Tehran kwa ajili ya shughuli za mazishi zinazotarajiwa kuvutia hadi waombolezaji milioni 20.
-
Kwa nini Iran inafungamanisha mazungumzo ya amani na usitishaji kamili wa mapigano nchini Lebanon
Jul 03, 2026 11:11Katika hali ya sasa ya mgogoro wa Mashariki ya Kati, suala la Lebanon limeibuka kama moja ya mihimili mikuu na muhimu katika mazungumzo ya kidiplomasia na vyombo vya habari. Katika uwanja huu, sisitizo la Iran la kusitishwa kikamilifu uvamizi wa utawala haramu wa Israel nchini Lebanon kama sharti la mazungumzo na Washington limeibua maswali mengi miongoni mwa wachambuzi wa kikanda na kimataifa. Msimamo huu sio hitajio la kimkakati tu bali ni sehemu ya mantiki pana ya kimkakati ya sera za kigeni
-
Iran yaonya mataifa ya Ghuba ya Uajemi baada ya kikao kilichosimamiwa na Marekani nchini Bahrain
Jul 03, 2026 09:00Iran imetoa onyo kwa nchi za kikanda kuwa zichukue tahadhari ya juu dhidi ya mipango ya usalama inayoongozwa na Marekani, ikisema kuwa nchi hizo zisizahau athari za uvamizi wa kijeshi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel uliovuruga usalama katika ukanda mzima wa Asia Magharibi.
-
Wapalestina wasisitiza haki ya kujilinda huku Gaza ikitimiza siku 1,000 za mauaji ya kimbari
Jul 03, 2026 08:25Makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina yamesisitiza kuhusu “haki ya Wapalestina kupinga uvamizi kwa namna yoyote ile” na kukataa “usimamizi wowote wa kigeni” katika mambo ya ndani ya Palestina, wakati Gaza ikifikisha siku ya 1,000 ya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala katili Israel ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina wasipungua 73,000.
-
Mamilioni wanatarajiwa shughuli ya kumuaga Kiongozi Shahidi nchini Iraq
Jul 03, 2026 07:24Mamilioni ya waumini wanatarajiwa kufurika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq kushiriki katika shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
-
Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaanza Tehran
Jul 03, 2026 06:35Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza awamu ya kwanza ya taratibu za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, huku viongozi wa kimataifa na wanazuoni wa kidini wakifika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini maarufu kama Mosalla mjini Tehran kutoa heshima zao za mwisho.