Nov 03, 2023 04:13 UTC
  • Wanajeshi 18 wa utawala haramu wa Israel waangamizwa katika operesheni ya ardhini Gaza

Jeshi la utawala haramu wa Israel limetangaza kuwa, wanajeshi wake 18 wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya katika operesheni yao ya ardhini huko Gaza Plestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, katika siku ya 27 ya operesheni ya kimbunga ya Al-Aqsa, viongozi wa utawala wa Kizayuniwamethibitisha kuwa idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa katika operesheni ya ardhini huko Gaza imeongezeka na kufikia 18.

Jeshi la Israel limetangaza pia kuwa wanajeshi wanne wa Israel walijeruhiwa vibaya wakati wa operesheni za ardhini kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo, Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni amesema: Idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa tangu kutekelezwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa imefikia 332 na idadi ya mateka huko Gaza imefikia watu 242 ambapo wengi wa mateka hao wa utawala wa Kizayuni wako hai.

Katika upande mwingine, vyombo vya habari vya Palestina vinaripoti juu ya kuendelea kwa mapigano makali ya ardhini katika maeneo ya Zeitoun, mashariki mwa Khan Yunis, kaskazini magharibi mwa Ukanda wa Gaza na kando kando mwa kitongoji cha Netzarim kilichoko kusini magharibi mwa mji wa Gaza.

Wakati huo huo, Batalioni za al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) sambamba na wapiganaji wa Saya al-Salam tawi la kijeshi la Harakati ya Jihadul Islami  zimefanya mashambulizi makubwa dhidi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa kaskazini-magharibi na kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Tags