Nov 25, 2023 13:03 UTC
  • Qais al-Khazali
    Qais al-Khazali

Kiongozi wa harakati ya muqawama ya Iraq amesema kuwa, vikosi vya majeshi ya Marekani havina nia ya kuondoka katika nchi hiyo ya Kiarabu na vinahalalisha uwepo wao kinyume cha sheria kwa kutumia kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh ambalo limekwishakufa na kutoweka.

Qais al-Khazali, Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama ya Asa'ib Ahlul Haq nchini Iraq ambayo ni sehemuu ya Vikosi vya Kupambana na Ugaidi vya (PMU) au al Hashd al-Sha'abi, ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na televisheni ya al-Ahad.

Khazali amesema: "Wamarekani hawataki kuondoka Iraq, na wakati  serikali inapochukua uamuzi wa kuwafukuza, wanatuma ujumbe wa vitisho wa kisiasa."

Kiongozi wa harakati ya Asa'ib Ahlul Haq amesema kuna "magaidi 700 tu wa Daesh katika ardhi ya Iraq," na kwamba lengo kuu la muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani ni "kulinda usalama wa taifa wa Marekani, ambao unahusishwa na utawala wa Kizayuni."

Khazali amesisitiza kuwa Iraq haihitaji uwepo wa vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani ili kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya safu za kundi la kigaidi la Daesh.

Amesema Iraq ni nchi yenye nguvu na ina jeshi na utaalamu ambao nchi nyingi za eneo la Magharibi mwa Asia hazina.

Wapiganaji wa al Hashd al-Sha'abi

Khazali pia amesema kwamba kuwepo kwa vikosi vya Marekani vinavyokalia kwa mabavu ardhi ya Iraq kunakiuka katiba ya nchi hiyo kwa sababu kuanzisha kambi za kijeshi za kigeni katika ardhi ya Iraq sio sehemu ya ombi la Iraq la msaada wa kimataifa ili kukabiliana na ugaidi katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Tags