Dec 02, 2023 10:42 UTC
  • Yemen: Silaha zetu zitaendelea kuupiga utawala wa Kizayuni wa Israel

Mjumbe wa ngazi za juu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, silaha za nchi yake zimeelekezwa kwa adui Mzayuni ambaye ndiye adui nambari moja na kwamba utaendelea kuzitumia silaha hizo kuupiga utawala huo dhalimu.

Hayo yameripotiwa na televisheni ya Al Mayadeen ambayo imemnukuu Muhammad Ali al Houthi, mmoja wa viongozi waandamizi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen akisema hayo na kusisitiza kuwa, Saudi Arabia inapaswa kuuorodhesha utawala wa Kizayuni katika magenge ya kigaidi.

Kiongozi huyo wa Yemen ameongeza kuwa, baada ya utawala wa Kizayuni kuanzisha wimbi jipya la jinai zake dhidi ya wananchi wa Ghaza, serikali za nchi za Kiarabu zimeishia tu kuitisha vikao na mikutano ya kulaani kwa maneno tu jinai hizo.

Kwa upande wake, muqawama wa Palestina umejibu jinai hizo mpya za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza huku Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ikisema kuwa, wa kubebeshwa dhima na lawama za kuanza tena mapigano ni Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Utawala wa Kiziayuni unafanya jinai zisizo na kifadni dhidi ya wananchi wa Ghaza

 

Televisheni ya Al Mayadeen imetangaza kuwa, jana Ijumaa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilishambulia kundi la wanajeshi wa Israel na kuwasababishia hasara kubwa. Muqawama wa Palestina nao umeendelea kukabiliana kishujaa na vilivyo na uvamizi wa jeshi la Israel katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza hasa kwenye eneo la al-Tawam la kaskazini magharibi mwa mji wa Ghaza.

Jana asubuhi, utawala wa Kizayuni ulianzisha tena jinai zake za kuua kikatili na kwa umati watu wasio na hatia kwenye maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza, baada ya kukwamisha mazungumzo ya kuendeleza usimamishaji vita kati yake na HAMAS. 

Takwimu za karibuni kabisa zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina zinaonesha kuwa, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi kuanzia jana hadi leo ni zaidi ya 200 na waliojerushiwa ni zaidi ya 589 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo. 

Tags