Feb 18, 2024 03:00 UTC
  • Kiongozi wa HAMAS: Israel inabeba dhima ya kukwama mazungumzo ya kusitisha vita

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unawajibika kwa kushindwa kupiga hatua mazungumzo na kufikia makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya "Al-Mayadeen", Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas ameongeza kuwa, muqawama hautaridhika na chochote isipokuwa kusitishwa kikamilifu uchokozi, kujiondoa kikamilifu jeshi vamizi la Kizayuni kutoka ukanda wa Gaza, na kuondolewa kikamilifu mzingiro wa kidhalimu.

Akibainisha kuwa katika kubadilishana wafungwa, kuachiliwa kwa mateka wa zamani kutapewa kipaumbele, alisema, harakati hii inaachukua hatua kwa uwajibikaji katia mazungumzo na katu haitapuuza kujitolea muhanga na mafanikio ya muqawama.

Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Hamas ameeleza kuwa, njia zote zitatumika kuzima hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Hali ya kibiinadamu Rafah ni mbaya sana

 

Wakati huo huo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Anthony Blinken amesema akiunga mkono Wazayuni na jinai zao kwamba bado haiwezekani kufikia makubaliano ya usitishaji vita kati ya Tel Aviv na harakati ya Hamas.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya katika Mkutano wa Usalama wa Munich kuhusu kuanguka kwa kibinadamu kutokana na yanayojiri katika eneo la Rafah la Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika Mkutano wa Usalama wa Munich kwamba: "Aina yoyote ya shambulio dhidi ya Rafah itasababisha maangamizi ya Wapalestina milioni moja na laki tano walioko katika eneo hilo."

Tags