Feb 25, 2024 09:55 UTC
  • Ngome za Israel zanyeshewa kwa 'mvua' ya makombora ya Hizbullah

Wanajihadi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebaon wameshambulia kwa makombora na maroketi kambi kadhaa za utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu usiku wa kuamkia leo.

Shirika la habari la Shehab limeripoti kuwa, Hizbullah imezipiga kwa makombora ngome kadhaa za utawala wa Kizayuni katika kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Kiryat Shamona, kaskazini mwa  ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Ripoti hiyo imeleeza kuwa, wanamapambano wa Hizbullah wameshambulia pia kambi ya wazayuni ya Batalioni ya Beit Hillel ya Brigedi ya 769 ya Eneo la Mashariki kwa makombora aina ya Katyusha.

Kadhalika mashambulizi mengine ya Hizbullah dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwenye mipaka ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni yamelenga kambi ya kijeshi ya Israel ya Azurit kwa makombora ya Burkan.

Taarifa ya Hizbullah ya Lebanon imeeleza kuwa, mashambulizi yake hayo ya kulipiza kisasi na ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina katika Ukand wa Gaza, yamewasababishia hasara kubwa wanajeshi makatili wa Israel. 

Nalo shirika la habari la Sputnik limesema makombora ya Hizbullah yamelenga kwa usahihi mkubwa maeneo zaidi ya 8 ya jeshi la utawala haramu wa Israel sanjari na kutekeleza kifaru cha utawala huo pandikizi katika mpaka wa kusini wa Lebanon.

Hadi hivi sasa makumi ya maelfu ya walowezi wa Kizayuni wamekimbia kutoka kwenye vitongoji vya Kizayuni karibu na mpaka wa Lebanon kwa kuhofia vipigo kutoka kwa Hizbullah. 

Mashambulizi ya karibu kila siku ya Hizbullah ya Lebanon dhidi ya Wazayuni ni ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu na wasio na ulinzi wa Palestina hasa wakazi wa Ukanda wa Gaza wanaoendelea kuuawa kinyama na Wazayuni.

Tags