Mar 21, 2024 02:53 UTC
  • Muqawama wa Iraq washambulia uwanja wa ndege Tel Aviv

Kwa mara nyingine tena wanamuqawama wa Iraq wameshambulia Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion katika mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, Tel Aviv.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, Muqawama wa Kiislamu wa Iraq jana asubuhi ulishambulia kwa droni uwanja huo wa ndege wenye shughuli nyingi mjini Tel Aviv, ili kuonyesha uungaji mkono kwa Wapalestina wa Gaza. 

Hakuna maelezo yaliyotokea kuhusu ukubwa wa uharibifu na maafa yaliyosababishwa na operesheni hiyo ya ndege zisizo na rubani ya wanamuqawama wa Iraq.

Makundi ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq yametangaza kuwa yanaendelea kuyashambulia maeneo mbalimbali ya utawala wa Kizayuni kwa kutumia droni, na kwamba mashambulizi hayo yataendelea hadi Israel itakapokomesha hujuma zake dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Shambulio la droni

Hivi karibuni, Makundi ya Muqawama ya Iraq yalitumia droni kukipiga kwa makombora kituo cha kemikali cha bandari ya Haifa ndani ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Kabla ya hapo pia, wanajihadi wa Iraq walishambulia Uwanja wa Ndege wa Rash Pina ulioko katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu la Al-Jalil.

Katika siku za karibuni pia, kambi za kijeshi za Marekani zimeshambuliwa mara kadhaa na ndege zisizo na rubani na roketi huko Iraq na Syria.  

Tags