May 04, 2019 02:52 UTC
  • Wanaharakati wa haki za binadamu wakusanyika mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia Paris kulaani jinai za Aal Saud

Kundi la wanaharakati wa msuala ya haki za binadamu limekusanyika tena mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Paris Ufaransa na kulaani jinai ya hivi karibuni ya Aal Saud ya kuwanyonga raia 37 wa nchi hiyo.

Kanali ya Televisheni ya al-Akhbariya ya Syria inaripoti kuwa, wanaharakati hao waliokusanyika mbele vya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Paris wamelaani hatua ya utawala wa kifamilia wa Aal Saudia ya kuwanyonga kwa umati raia wa nchi hiyo. 

Mmoja wa washiriki wa mkusanyiko huo amewaambia wanaandishi wa habari kwamba, utawala wa Saudi Arabia unaufadhili ugaidi wa kimataifa na umekuwa ukitenda kila aina ya jinai na wakati huo huo umekuwa ukifanya njama za kuvuruga amani na usalama wa Asia Magharibi na ulimwengu kwa ujumla. 

Baadhi ya waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango na maberamu mbalimbali yenye jumbe za kulaani jinai za Saudia huku wengine wakizipaza sauti wakitaka utawala huo ukomeshe jinai zake.

 

Mfalme na mrithi wa kiti cha ufalme Saudi Arabia wakiteta jambo

Mkusanyiko huo umefanyika sambamba na kuendelea kushuhudiwa  malalamiko ya walimwengu katika kila kona ya dunia dhidi ya jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Saudia ya kuwanyonga kwa umati raia 37 wa nchi hiyo kwa tuhuma zisizo na msingi wowote.

Hivi karibuni watawala wa Aal-Saud waliwanyonga kwa kuwakata vichwa watu 37, aghalabu yao wakiwa Waislamu wa madhehebu ya Shia na kisha kuanika mwili wa mmoja wa Waislamu hao waliowafanyia ukatili huo kwenye kigingi hadharani kwa ajili ya kutazamwa na umati.

Tags