-
Kigali: Mwenyeji wa kikao cha mameya wa miji ya Francophone + Sauti
Jul 21, 2021 11:30Meya wa miji mikuu ya nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa wameyahimiza mataifa wanachama hasa yale yaliyoko kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika kulipa kipaumbele suala la kuwaelimisha wananchi wao kuhusu elimu ya uzazi wa mpango. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.
-
Waandishi Tanzania watakiwa kutumia vizuri kalamu zao kutatua migogoro + Sauti
Jul 15, 2021 09:07Waandishi wa habari nchini Tanzania wametakiwa kutumia vizuri kalamu zao kwa ajili ya kuimarisha amani na kutatua migogoro katika jamii ikiwemo ya wakati wa uchaguzi. Harith Subeit na maelezo zaidi kutoka Zanzibar.
-
Rwanda yatangaza siku kumi za Lockdown kufuatia kuongezeka maambukizi ya Covid-19 + Sauti
Jul 15, 2021 08:06Serikali ya Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje kwa muda wa siku 10 katika mji mkuu, Kigali na wilaya nane baada ya kuripotiwa ongezeko la idadi ya vifo na wagonjwa wa COVID-19 nchini humo.
-
Rais Mwinyi wa Zanzibar aahidi mazuri zaidi kupitia uchumi buluu + Sauti
Jun 13, 2021 03:32Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa, serikali ya awamu ya nane ya Zanzibar ina dhamira ya dhati ya kupanua wigo wa matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake ili kujenga uchumi wa buluu ulio imara kwa taifa. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit na maelezo zaidi.
-
HAMAS: Umma wa Kiislamu unapaswa kuungana kukomesha ugaidi wa Israel + Video
Jun 10, 2021 02:22Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Umma wa Kiislamu una jukumu la kuungana na kuwa kitu kimoja kama unataka kweli kukikomboa Kibla chao cha Kwanza yaani Msikiti wa al Aqsa na kukomesha jinai na ugaidi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa azabwa kibao + Video
Jun 08, 2021 22:01Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amezabwa kibao wakati akiwa ziarani kusini mashariki mwa nchi hiyo. Katika kuonesha kuwa bado watu wanampenda, rais huyo anayeshindwa kuficha chuki zake dhidi ya Uislamu, alikwenda haraka kuwapa mikono watu waliokuwa wamesimama pembeni. Mtu wa kwanza kumpa mkono ametumia fursa hiyo hiyo kumzaba kibao.
-
Pogba na Diallo wakiwa na bendera ya Palestina waonyesha kuwaunga mkono Wapalestina +VIDEO
May 19, 2021 03:55Paul Pogba nyota wa timu ya soka ya Manchester United ya Uingereza na mwenzake Ahmad Diallo walionekana jana baada ya mechi wakiwa na bendera ya Palestina na kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina wanaokabiliwa na hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Mamia ya Maelfu ya Wayemen waandamana kuwaunga mkono ndugu zao Wapalestina + Video
May 17, 2021 22:21Maandamano makubwa ya kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina na mapambano yake ya ukombozi, yamefanyika huko San'a, mji mkuu wa Yemen.
-
Picha ya aliyefanya uharibifu katika kituo cha nyuklia cha Iran, yasambazwa + Video
Apr 17, 2021 08:04Wizara ya Masuala ya Kijasusi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesambaza picha ya aliyefanya uharibifu katika kituo cha nyuklia cha Natanz hivi karibuni humu nchini.
-
Jaribio la mapinduzi Jordan, makumi ya viongozi watiwa mbaroni + Video
Apr 03, 2021 22:38Duru za habari usiku wa kuamkia leo zimetangaza habari ya kutiwa mbaroni makumi ya viongozi wa ngazi za juu wa Jordan kwa tuhuma za kujaribu kufanya mapinduzi dhidi ya mfalme Abdallah II.