-
SAUTI, Serikali ya Zanzibar yafurahishwa na ziara ya ujumbe wa bunge la Iran, mahusiano pande mbili yanaimarika
Apr 19, 2018 12:33Serikali ya Zanzibar imeonyesha kufurahishwa kwake na ziara ya ujumbe wa bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran visiwani humo.
-
Maafa ya mvua za Masika visiwani Zanzibar + Sauti
Apr 18, 2018 13:36Zaidi ya watu elfu kumi wamekosa makazi visiwani Zanzibar kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku nyumba 16 zikipata athari za kuvunjika kuta na kusababisha baadhi watu kuhama makazi yao. Mwandishi wetu Harith Subeit ametuandalia ripoti maalumu kuhusu habari hiyo...
-
Serikali ya Uganda yatakiwa kuheshimu haki za binadamu + Sauti
Apr 18, 2018 13:32Tume ya haki za binadamu nchini Uganda imeshauri vyombo vyote vya serikali kuheshimu haki za washukiwa kwa vyovyote vile. Mwandishi wetu wa Kampala Kigozi Ismail ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo...
-
SAUTI, Mafuriko yaendelea kuyakumba maeneo yote ya Afrika Mashariki, Rwanda yapoteza watu 42
Apr 17, 2018 12:04Serikali ya Rwanda imethibitisha vifo vya watu 41 waliofariki dunia kutokana na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini humo.
-
DRC yataka ipewe fedha zilizokusanywa Uswisi + Sauti
Apr 16, 2018 05:32Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetaka ipewe fedha zilizokusanywa na wafadhili Ijumaa Uswisi ingawa ilisusia kikao hicho. Mossi Mwasi ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo
-
Waislamu Uganda watakiwa kushikamana na dini yao + Sauti
Apr 15, 2018 02:04Waislamu nchini Uganda na duniani kiujumla wametakiwa kushikamana na dini yao kama njia ya kuokoka duniani na Akhera.
-
Serikali ya CAR yakata njia zote za mawasiliano ya simu + Sauti
Apr 15, 2018 01:58Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui umeingia katika giza totoro kufuatia serikali kukata njia zote za mawasiliano kutokana na hali mbaya ya usalama. Mwandishi wetu Mosi Mwasi ametuandalia ripoti maalumu kuhusu habari hiyo...
-
Zitto Kabwe: Watu wa Kigoma hawashindwi vita, hawatokubali kuonekana sio raia wa Tanzania (sauti)
Apr 13, 2018 03:07Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amelaani vitendo vya kupotezwa watu vinavyoendelea kujiri nchini Tanzania kikiwemo kitendo cha kupotezwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani humo, Simon Kangue.
-
Mkuu wa UNHCR amaliza ziara yake nchini Burundi + Sauti
Apr 13, 2018 02:16Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa amemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Burundi ambapo amejadiliana na Rais Pierre Nkurunziza suala la kurejeshwa wakimbizi wa Burundi waliokimbila nchi jirani. Mwandishi wetu Hamida Issa ametuandalia ripoti maalumu kuhusu ziara hiyo ya Filippo Grandi nchini Burundi
-
Watu 257 wapoteza maisha katika ajali ya ndege nchini Algeria + Video
Apr 11, 2018 09:18Televisheni ya serikali ya Algeria imetangaza kuwa, watu wasiopungua 257 wamepoteza maisha baada ya ndege ya kijeshi kuanguka katika uwanja wa ndege wa Boufarik, nje ya mji mkuu wa nchi hiyo, Algiers.