-
Kampeni zamalizika Uganda, uchaguzi Alkhamisi
Feb 17, 2016 03:33Nchini Uganda kampeni za uchaguzi zilimalizika Jumanne huku wagombea wa viti vya urais na ubunge wakijitayarisha kwa ajili ya upigaji kura siku ya Alkhamisi.
-
Serikali yazidi kuwabana wapinzani nchini Uganda
Feb 15, 2016 11:56Huku siku chache tu zikiwa zimebakia hadi kufanyika uchaguzi mkuu wa Februari 18 nchini Uganda, polisi ya nchi hiyo leo imemtia mbaroni na baadaye kuwachia Daktari Kizza Besigye, kiongozi wa chama cha upinzani cha cha FDC. Besigye amekamatwa na polisi wakati alipokuwa anakwenda kwenye mkutano wa hadhara katika wilaya yenye shughuli nyingi, jijini Kampala.
-
Tume: Uchaguzi nchini CAR umefanyika kwa amani
Feb 15, 2016 11:56Uchaguzi Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umefanyika katika mazingira ya utulivu na amani.
-
Duru ya pili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati yafanyika leo
Feb 14, 2016 03:34Duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati inafanyika leo ambayo inaonekana kuwa ni hatua muhimu ya kurejesha utawala wa kidemokrasia na kumaliza miaka kadhaa ya vita vilivyoleta mpasuko na mgawanyiko nchini humo.
-
Rais wa Liberia yuko nchini Uganda kwa ajili ya uchaguzi
Feb 13, 2016 22:22Rais Ellien Johnson Sirleaf wa Liberia yuko nchini Uganda kufuatilia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki unliopangwa kufanyika wiki ijayo Februari 18.
-
Uchaguzi wa rais Benin waahirishwa hadi mwezi ujao
Feb 13, 2016 11:55Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Benin ambao ulitazamiwa kufanyika mwishoi mwa mwezi huu umeahirishwa hadi mwezi ujao.
-
Chama cha CUF nchini Tanzania chakubali kurudi kwenye mazungumzo lakini…
Feb 12, 2016 23:53Chama cha Wananchi CUF cha nchini Tanzania kimekubali kurudi kwenye mazungumzo ya kuutafutia ufumbuzi wa amani mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar, kwa sharti kwamba, mchakato wa uchaguzi wa marudio usimamishwe.
-
Kaduma: Ni vyema Sheni angekubali kushindwa
Feb 10, 2016 11:54Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Ibrahim Kaduma ameungana na wanasiasa na shakhsia wengine mashuhuri nchini humo ambao wanapinga kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar kwa maelezo kuwa maridhiano baina ya pande zinazopingana yana nafasi nzuri ya kutatua mgogoro uliopo.
-
161 kugombea viti vya Baraza la Wataalamu Iran
Feb 10, 2016 11:52Idara Kuu ya Usimamizi wa uchaguzi wa Iran imesema wagombea 161 wameidhinishwa na Baraza la Walinzi wa Katiba kuwania viti katika uchaguzi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.
-
Mwinyi kuongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi UG
Feb 09, 2016 11:35Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi ameteuliwa kuongoza timu ya waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye uchaguzi mkuu wa Uganda wa Februari 18.