-
Mahakama ya Zambia yaamua kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani iendelee
Apr 26, 2017 08:38Mahakama ya Zambia imeamua kuwa kesi ya uhaini inayomkablia kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema iendelee huku malumbano ya kisiasa yakitokota katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
-
Chanjo ya kwanza ya kinga ya homa ya Malaria kufanyiwa majaribio barani Afrika
Apr 24, 2017 10:36Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza leo kuwa chanjo ya kwanza ya kinga ya ugonjwa hatari wa homa ya malaria itafanyiwa majaribio katika bara la Afrika.
-
Kuanza maneva ya "Simba wa Afrika" nchini Morocco
Apr 22, 2017 07:23Maneva ya kijeshi yaliyopewa jina la "Simba wa Afrika" yameanza katika nchi ya Kiafrika ya Morocco yakishirikisha askari wa Jeshi la Majini la Marekani na wanajeshi 1300 kutoka nchi nyinginen 11.
-
Benki ya Dunia ina matumaini na ustawi wa kiuchumi Afrika
Apr 21, 2017 02:12Benki ya dunia inasema kasi ya ukuaji wa uchumi barani Afrika inaridhisha mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo uchumi wa bara hilo uliporomoka kwa kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha miongo miwili.
-
SAUTI: Vijana Rwanda watakiwa kujihadhari na ukoloni mamboleo
Apr 16, 2017 03:12Serikali ya Rwanda imewataka raia wake hasa vijana kutambua hila na njama za ukoloni mamboleo unaofanywa na nchi za kigeni hasa zile za Magharibi. Kwa upande wa vijana wakati huu ni ule wa kuzipenda nchi zao za Kiafrika na kuepuka kufikiria nchi zilizoendelea. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.
-
Uchumi wa nchi za kusini mwa Sahara waitia wasi wasi Côte d’Ivoire
Apr 06, 2017 03:07Serikali ya Côte d’Ivoire imeoyesha wasi wasi juu ya mwendelezo wa kushuka kiwango cha uchumi wa nchi za kusini mwa Sahara, barani Afrika.
-
Kupambana na ugaidi, lengo la kongamano la usalama barani Afrika
Apr 04, 2017 08:05Viongozi wa masuala ya intelijensia na usalama kutoka nchi 30 za Kiafrika wanakutana mjini Khartoum, Sudan katika kikao cha siku tatu kwa lengo la kuchunguza mikakati ya kupambana na vitisho vipya na ongezeko la ugaidi barani humo.
-
US$ Milioni 255 zahitajika kuwasaidia watoto kukabiliana na njaa Afrika, Yemen
Mar 30, 2017 02:12Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, watoto takriban milioni 1.4 nchini Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa.
-
Tahadhari kuhusu hali ya mgogoro katika nchi za mashariki mwa Afrika
Mar 27, 2017 07:31Mgogoro wa ukame katika eneo la mashariki mwa Afrika umeulazimisha Umoja wa Mataifa kutoa onyo kuhusiana na hatari ya janga la wakimbizi kwenye eneo hilo.
-
UN yaanzisha kampeni mpya ya kutokomeza Polio Afrika
Mar 25, 2017 03:13Kampeni ya chanjo ya aina yake kuwahi kufanyika katika bara la Afrika dhidi ya polio itatoa chanjo kwa watoto milioni 116 wiki ijayo katika nchi 13 za Afrika Magharibi na Kati, limesema Shirika la Afya Duniani, WHO na Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF.