Uchunguzi wa kielimu waonyesha uzalishaji elimu barani Afrika uko chini sana
https://parstoday.ir/sw/news/world-i30090-uchunguzi_wa_kielimu_waonyesha_uzalishaji_elimu_barani_afrika_uko_chini_sana
Uchunguzi mpya uliofanywa na jopo la wahadhiri nchini Ufaransa, umebaini kuwa uzalishaji elimu katika mataifa ya Kiafrika uko katika kiwango cha chini ikilinganishwa na maeneo mengine ya dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 05, 2017 22:52 UTC
  • Uchunguzi wa kielimu waonyesha uzalishaji elimu barani Afrika uko chini sana

Uchunguzi mpya uliofanywa na jopo la wahadhiri nchini Ufaransa, umebaini kuwa uzalishaji elimu katika mataifa ya Kiafrika uko katika kiwango cha chini ikilinganishwa na maeneo mengine ya dunia.

Uchunguzi huo uliofanywa na wahadhiri wa jiografia katika Chuo Kikuu cha Toulouse nchini Ufaransa kuhusiana na suala la uzalishaji elimu duniani, umeonyesha nafasi ya mwisho kabisa ya bara Afrika. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, Afrika bado ina kiwango duni cha elimu na kwamba nchi za kusini na kaskazini mwa bara hilo ndizo zina uafadhali wa kielimu ikilinganishwa na mataifa ya maeneo mengine. 

Baadhi ya wanachuo barani Afrika

Kwa mfano tu, ripoti iliyotolewa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) iliitaja Cameroon kuwa iliyoshika nafasi ya nne mwaka 2010, nafasi ya tatu mwaka 2012 na nafasi ya nne tena mwaka 2013 katika masuala ya uvumbuzi. Kadhalika ripoti hiyo iliitaja Kenya kuwa iliyoshika nafasi ya saba kati ya mwaka 2010 na 2013. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, bara la Ulaya linashika nafasi ya kwanza kwa mtazamo wa uzalishaji wa makala za kielimu duniani, huku Marekani na Uchina zikishika nafasi ya pili katika uga huo.