Watu 20 wafariki katika ajali ya barabarani mashariki mwa Zambia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29514-watu_20_wafariki_katika_ajali_ya_barabarani_mashariki_mwa_zambia
Watu 20 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa likitokea kwenye mji mkuu wa Zambia, Lusaka, kupoteza mwelekeo na kupinduka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 24, 2017 09:36 UTC
  • Watu 20 wafariki katika ajali ya barabarani mashariki mwa Zambia

Watu 20 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa wakati basi lililokuwa likitokea kwenye mji mkuu wa Zambia, Lusaka, kupoteza mwelekeo na kupinduka.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Esther Mwaata-Katongo amesema, ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa tatu usiku kwa saa za eneo hilo baada ya dereva wa basi kushindwa kukata kona, na kusababisha basi hilo kupinduka. Amesema miongoni mwa marehemu ni watoto watatu, wanaume sita na wanawake watatu.

Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Zambia, ambapo mwaka jana, serikali ilipiga marufuku magari yote kusafiri usiku ili kupunguza ajali hizo.

Ajali ya hivi karibuni Arusha, Tanzania

Katika wiki za hivi karibuni kumetokea ajali kadhaa za barabarani Afrika ambapo nchini Kenya watu 20 walipoteza maisha katika ajali ya  barabara ya Nairobi na Nakuru. Aidha nchini Tanzania watoto 32 wa shule walifariki dunia eneo la Arusha.

Ajali nyingi barani Afrika hutokea kutokana na kutozingatia sheria za usalama barabarani hasa mwendo wa kasi na pia barabara zenye viwango duni.