-
Afrika Kusini nayo yajibu mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani dhidi yake
Aug 22, 2018 09:57Serikali ya Afrika Kusini imelalamikia vikali mashinikizo ya serikali ya Marekani dhidi ya uchumi wa nchi hiyo na imeamua kutopeleka tena mifugo yake ya jamii ya kuku huko Marekani kama njia ya kupinga ushuru mpya ziliowekewa bidhaa zake na serikali ya Donald Trump.
-
ANC yaitaka serikali itwae ardhi kwa wale wote wanaomiliki zaidi ya hekta elfu 12 nchini Afrika Kusini
Aug 15, 2018 22:03Mwenyekiti taifa wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha (ANC) amenukuliwa wiki hii akisema kuwa serikali inapasa kuchukua ardhi za wale wanaomiliki zaidi ya hekta elfu 12 bila ya kuwalipa fidia; matamshi ambayo yamepelekea kupungua thamani ya pesa ya nchi hiyo.
-
Mahakama ya juu ya Afrika Kusini yaagiza kuondolewa Mwendesha Mashtaka Mkuu aliyeteuliwa na Zuma
Aug 14, 2018 03:49Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini imebatilisha uteuzi wa Mwendesha Mashtaka Mkuu ambaye alipewa kazi baada ya rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma kumfuta kazi aliyekuwepo kabla yake. Mahakama hiyo imetaka Mwendesha Mashtaka Mkuu wa zamani arejeshwe kazini katika muda wa siku 90.
-
Afrika Kusini inaendelea kuziuzia Saudia, Imarati silaha zinazoua Wayemen
Jul 27, 2018 03:21Ripoti ya kila mwaka ya Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti Silaha nchini Afrika Kusini (NCACC) inaonesha kuwa, Saudi Arabia na Imarati zinaendelea kurundika silaha zinazonunua kutoka nchi hiyo ya Kiafrika, na ambazo zinatumika mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen.
-
China, Afrika Kusini zatoa wito wa kushirikiana kibiashara katika mkutano wa BRICS
Jul 25, 2018 09:53China na Afrika Kusini leo zimezitolea wito nchi wenza zinazounda kundi la BRICS kupambana na kile kilichotajwa na nchi hizo kuwa ni hatua ya kuvilinda na ushindani wa nje viwanda vya ndani vya nchi moja kupitia ushuru wa forodha.
-
Madereva 11 wa taxi Afrika Kusini wapigwa risasi na kuuawa wakitoka mazishini
Jul 22, 2018 03:02Maderva 11 wa taxi wamepigwa risasi na kuuawa nchini Afrika Kusini wakati wakirejea mjini Johannesburg baada ya kuhudhuria mazishi ya mwenzao katika eneo la Kwa-Zulu Natal.
-
Afrika Kusini yasema itaendelea kulaani jinai za Israel huko Palestina
Jul 08, 2018 23:22Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa mashambulizi yanayoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina hususan katika Ukanda wa Gaza hayakubaliki na kwamba kwa sababu hiyo balozi wake hatarejea Tel Aviv.
-
Waislamu Afrika Kusini walaani mauaji ya kikatili msikitini
Jun 15, 2018 11:07Baraza la Kisheria la Waislamu la Afrika Kusini (MJC) limelaani vikali shambulizi la kikatili lililotokea Alhamisi katika eneo la Malmesbury karibu na mji wa Cape Town, na kusababisha vifo vya waumini wawili wa Kiislamu na wengine wawili kujeruhiwa.
-
Zarif arejea Tehran kutokea Afrika Kusini
Jun 14, 2018 10:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amerejea hapa Tehran leo asubuhi baada ya kumaliza ziara rasmi nchini Afrika Kusini ambako alionana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mbalimbali wa nchi hiyo.
-
Watu wawili wauawa kwa kudungwa visu msikitini nchini Afrika Kusini
Jun 14, 2018 03:42Kwa akali watu wawili wamethibitishwa kuuawa kwa kudungwa visu wakiwa msikitini, baada ya mtu mmoja kuvamia eneo hilo la ibada nchini Afrika Kusini.