Iran na Afrika Kusini kustawisha uhusiano wao wa kiulinzi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i48798-iran_na_afrika_kusini_kustawisha_uhusiano_wao_wa_kiulinzi
Mkuu wa masuala ya kimataifa wa Wizara ya Ulinzi ya Iran na Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini wamesisitizia kustawishwa ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi kati ya nchi mbili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 15, 2018 00:16 UTC
  • Iran na Afrika Kusini kustawisha uhusiano wao wa kiulinzi

Mkuu wa masuala ya kimataifa wa Wizara ya Ulinzi ya Iran na Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini wamesisitizia kustawishwa ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi kati ya nchi mbili.

Brigedia Jenerali Mohammad Ahadi, mkuu wa masuala ya kimataifa wa Wizara ya Ulinzi ya Iran, ambaye ameeleka mjini Pretoria, Afrika Kusini kuhudhuria kikao cha pili cha tume ya pamoja ya ushirikiano wa kiulinzi kati ya Iran na Afrika Kusini, amesema, sifa maalumu za kiiopolitiki na irada ya kisiasa waliyonayo viongozi wa Iran na Afrika Kusini, zinaandaa mazingira mwafaka ya kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili hususan katika uga wa ulinzi.

Brigedia Jenerali Ahadi ameyasema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini Bi Nosiviwe Mapisa-Nqakula, ambapo sambamba na kuashiria chimbuko la kuenea ugaidi katika eneo la Magharibi ya Asia, amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko mstari wa mbele katika kupambana na ugaidi na misimamo ya kufurutu mpaka katika eneo hili. Aidha ameeleza kusikitishwa na maafa ya kibinadamu nchini Yemen na kimya cha jumuiya za kimataifa kuhusiana na maafa hayo pamoja na siasa za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za Marekani katika uga wa kimataifa ikiwemo hatua yake ya kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Image Caption

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini Bi Nosiviwe Mapisa-Nqakula ameashiria sera za kistratejia za Afrika Kusini katika kupanua uhusiano wake na nchi zenye misimamo huru na muelekeo sawa na wa nchi hiyo na kueleza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliihami na kuiunga mkono Afrika Kusini katika kipindi kigumu.

KIkao cha pili cha tume ya pamoja ya ushirikiano wa kiulinzi kati ya Iran na Afrika Kusini kilifanyika tarehe 9 hadi 11 ya mwezi huu wa Oktoba huko Pretoria, mji mkuu wa Afrika Kusini.../