Waasi wa Kikristo wenye mfungamano na genge la kigaidi la anti-Balaka wameua Waislamu 25 ndani ya msikiti katika mji wa Kembe wa kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kushadidi zaidi mgogoro wa nchi hiyo.
Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeeleza wasiwasi mkubwa ilionao kutokana na kuzidi kuwa mbaya hali ya kibinadamu katika maeneo ya magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Watu 25 wameuawa katika mapigano mapya huko Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) huku waziri wa ulinzi nchini humo akifutwa kazi kutokana na ongezeko la machafuko nchini humo.
Duru za usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati zimeripoti habari ya kujiri mapigano mapya kati ya waasi wa zamani wa kundi la Seleka katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.
Mapigano makali yameripotiwa kati ya makundi ya Seleka na Anti-Balaka katika mji wa Bria wa katikati mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuua zaidi ya watu 10.
Huku Umoja wa Mataifa ukionya juu ya uwepo wa viashiria vya kutokea mauaji ya kimbari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad ameiomba jamii ya kimataifa ichukue hatua za ziada kuhusiana na suala hilo.
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limeripoti kuwa, wafanyakazi wake kadhaa wameuawa katika shambulizi lililofanywa na waasi huko kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Shirika la Madaktari Wasio Mipaka limetangaza kuwa, Jamhuri ya Afrika ya Kati inakabiliwa na hali mbaya na ya hatari.
Mapigano yanayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha vifo vya watu wawili na kujeruhiwa wengine wanne.