Aug 17, 2017 02:37 UTC
  • Chad: Walimwengu wachukue hatua za haraka kuzuia mauaji ya kimbari CAR

Huku Umoja wa Mataifa ukionya juu ya uwepo wa viashiria vya kutokea mauaji ya kimbari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad ameiomba jamii ya kimataifa ichukue hatua za ziada kuhusiana na suala hilo.

Hissein Brahim Taha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad amesema kuwa, serikali ya N'Djamena na Stephen O'Brien, afisa wa masuala ya kibinaadamu wa Umoja wa Mataifa, wana wasiwasi mkubwa kutokana na hali ya mambo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Sambamba na Stephen O'Brien kuashiria suala hilo ameonya juu ya madhara yanayoweza kutokea kiusalama na kibinadamu katika ya eneo zima la katikati mwa Afrika hususan Chad ikiwa kutatokea mauaji hayo.

Wanachama wa kundi la kigaidi la Kikristo la Anti-Balaka nchini CAR

Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad ameyataka makundi tofauti ya CAR kujiepusha na vitendo ambavyo vitaitumbukiza nchi hiyo katika maafa makubwa.

Chad ina karibu wakimbizi elfu 74 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika katika machafuko mwishoni mwa 2013 baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé, machafuko ambayo yamekuwa yakiambatana na mauaji makubwa na uporajimali.

Tags