Dakta Tedros Adhanom Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema leo kuwa kuenea kwa maradhi ya Ebola katika mji mkuu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni jambo lenye kutia hofu hata hivyo akasema kuwa maandalizi ya kukabiliana na hali ya sasa yameboreka zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 2014 huko Magharibi mwa Afrika wakati ulivyoripotiwa mlipuko mkubwa wa homa hiyo hatari.
Wafanyakazi wa sekta ya afya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wataanza kupewa chanjo ya Ebola kesho Jumatatu katika juhudi za kuzuia kuenea ugonjwa huo hatari.
Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamelipatia idhini Shirika la Afya Duniani (WHO) kuingiza na kutumia nchini humo chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola. Hayo yameelezwa jana na Dakta Tedros Adhanom Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa WHO.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na taasisi za Umoja wa Mataifa zimeanza kutuma nchini humo timu za wataalamu ili kujaribu kuzuia kuenea maambukizi ya homa ya Ebola ambayo hadi sasa inashukiwa tayari imeshawaambukiza watu zaidi ya 30.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha juu ya uwezekano wa kuibuka tena ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Uganda imethibitisha kufariki dunia mtu mmoja kwa homa inayoenezwa na kirusi cha Marburg, homa ambayo huambatana na kuvuja damu sawa kabisa na homa ya Ebola. Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya wa nchi hiyo.
Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC idadi ya visa vinavyoshukiwa kuwa ni Ebola imeongezeka na kufikia 20.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, ugonjwa wa Ebola umezuka katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwamba, hadi sasa watu watatu wamefariki dunia kwa ugonjwa huo hatari.
Watu tisa wamepoteza maisha na wengine wanane bado wako hospitalini nchini Liberia baada ya kuibuka ugonjwa usiojulikana na kuwakumba watu 17 tangu siku ya Jumatatu ya Aprili 24.
Utafiti uliochapishwa katika jarida la Lancet umeonyesha kuwa chanjo ya majaribio ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Ebola kwa jina la rVSV-ZEBOV inaonekana kuwa na athari kwa asilimia 100.