Oct 07, 2018 07:45 UTC
  • Visa vipya vya Ebola vyathibitishwa Kongo DR

Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imethibitisha habari ya kugunduliwa kwa kesi tano mpya za maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola katika mji wa Beni, mashariki mwa nchi.

Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa, idadi ya wahanga wapya wa Ebola nchini DRC imefikia 140, ambapo 108 miongoni mwao wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo hatarishi tangu mwezi Mei hadi sasa.

Kesi hizi mpya za Ebola nchini DRC zimeripotiwa katika hali ambayo, Julai 25, Wizara ya Afya nchini humo ilitangaza rasmi kwamba maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yamekomeshwa kikamilifu nchini humo, baada ya uchunguzi wa kina wa siku 42. 

Chanjo ya Ebola

Mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola ulianza tarehe 8 Mei mwaka huu katika mji wa Bikoro kwenye mkoa wa Équateur huko kaskazini magharibi mwa Kongo na baadaye maambukizi ya ugonjwa huo yalihamia katika mji wa Mbandaka ambao ndio makao makuu ya mkoa huo.

Itakumbwa kuwa, kuanzia mwishoni mwa mwaka 2013 hadi 2016 ugonjwa huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 11 na 300 katika baadhi ya nchi za magharibi mwa Afrika. 

Tags