Nov 30, 2018 04:33 UTC
  • WHO: Kesi 36 mpya za Ebola ziripotiwa DRC

Hatari wa kuenea ugonjwa habari wa Ebola imeongezeka huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na katika nchi zinazopakana nayo baada ya kesi nyingine 36 kugunduliwa karibu na mpaka wa nchi hiyo katika wiki iliyomalizikia kwenye Novemba 29.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema katika ripoti yake ya jana Alkhamisi kwamba, ktika kipindi cha baina ya tarehe 21 hadi 27 Novemba 2018, kumeripotia kesi 36 mpya za ugonjwa wa Ebola, 13 katika mji wa Beni, ti katika mji wa Katwa, sita Kalungunta, sita Butembo, moja Khondo na nyingine moja huko Oicha.

Shirika hilo limeongeza kuwa, hatari ya kuenea ugonjwa huo katika mikoa mingine ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni kubwa sawa kabisa na hata kuingia katika nchi jirani.

Kijana wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akipigwa chanjo ya kujikinga na Ebola

 

Mara hii mripuko wa ugonjwa hatari wa Ebola umeanzia katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri huko DRC ambayo inapakana na Uganda, Sudan Kusini, Rwanda, Burundi na Tanzania.

Wiki iliyopita kulitolewa tahari ya uwezekano wakuingia ugonjwa wa Ebola katika nchi za Sudan Kusini na Uganda, hata hivyo hadi hivi sasa hakuna kesi yoyote ya ugonjwa huo iliyoripotiwa kuingia kwenye nchi hizo jirani.

Hadi kufikia tarehe 27 Novemba 2018, kulikuwa kumeripotiwa kesi 422 za Ebola, 375 kati ya hizo zikiwa zimethibitishwa na 47 ni za kudhaniwa. Hadi tarehe hiyo, watu 242 walisharipotiwa kufariki dunia huko Kivu Kaskazini na Ituri.

Mfumuko mkubwa zaidi wa ugonjwa wa Ebola ulitokea baina ya Disemba 2013 na Aprili 2016 na kuua zaidi ya watu 11,000 katika nchi za magharibi mwa Afrika za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Tags