Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza habari ya kumalizika maambukizo ya homa hatari ya Ebola huko Guinea Conakry.
Serikali ya Liberia imechukua uamuzi wa kufunga mipaka yake na Guinea Konacry baada ya watu kadhaa kufariki dunia katika nchi hiyo jirani kwa homa ya Ebola.
Mripuko wa homa hatari ya Ebola nchini Guinea Conakry umesababisha vifo vya watu watano huku mamia ya wengine wakiaminika kuwa tayari wameambukizwa ugonjwa huo.
Shirika la Afya Duniani WHO limepeleka timu ya wataalamu Kusini mwa mkoa wa Nzérékoré nchini Guinea Conakry baada ya visa vipya viwili vya Ebola kubainika na kuthibitishwa katika maeneo ya kijijini.