Aug 21, 2018 07:40 UTC
  • Idadi ya wahanga wa homa ya Ebola yaongezeka DRC

Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilitangaza jana kwamba idadi ya wahanga wa wimbi jipya la kuenea ugonjwa wa Ebola nchini humo imeongezeka na kufikia watu 50.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kuinukuu wizara hiyo ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo ikisema kuwa, kati ya kesi 91 zilizoripotiwa katika vituo vya afya, imethibitika kuwa 64 kati yake ndizo za ugonjwa huo wa Ebola.

Wimbi jipya la maambukizi ya Ebola limeikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu tarehe 8 Mei mwaka huu na ulianzia katika mji wa Bikoro, mkoani Équateur, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo kubwa ya katikati mwa Afrika. 

Tafiti mbalimbali zinaendelea kufanyika kuutafutia suluhusho la kudumu ugonjwa hatari wa Ebola

 

Baada ya hapo ugonjwa huo ulienea hadi katika mji wa Mbandaka, katikati ya mkoa huo na kufika hadi mashariki mwa nchi.

Tangu mwaka 2014 hadi hivi sasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeshakumbwa mara tatu na wimbi la ugonjwa hatari wa Ebola.

Katika kipindi cha baina ya mwaka 2013 hadi 2016, virusi hatari vya Ebola vimechukua roho za karibu watu 11 elfu katika maeneo tofauti duniani.

Tags