-
Iran na Uganda zaazimia kupanua ushirikiano katika uga wa mawasiliano na teknolojia ya habari
May 02, 2024 07:51Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran ametangaza utayari wa taifa hili wa kushirikiana na Uganda katika miradi ya mawasiliano na teknolojia habari na uhamishaji wa taaluma hiyo kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.
-
Iravani: Madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran; juhudi za kuupotosha ulimwengu kuhusu jinai za Gaza
May 02, 2024 04:13Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameyataja madai ya uwongo ya Israel dhidi ya Iran kuwa ni juhudi zenye lengo la kupotosha mazingatio ya walimwengu kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
-
Iran yakaribisha kuendelea mazungumzo kati yake na Umoja wa Ulaya
May 02, 2024 04:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekaribisha na kuunga mkono kuendelea kufanyika mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Iran ili kusogeza mbele ushirikiano wa pamoja na kusema: Ushirikiano kati ya wakala wa IAEA na Iran upo katika njia nzuri.
-
Iran na Afrika ya Kati kuimarisha ushirikiano wa sekta ya madini
May 01, 2024 23:07Waziri wa Biashara Ndogo na za Kati wa Afrika ya Kati ametangaza utayarifu wa nchi yake wa kushirikiana kikamilifu na Iran katika uchimbaji madini.
-
Iran na Uganda kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo
May 01, 2024 03:48Mwenyekiti wa Kamisheni ya Viwanda na Madini ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inatilia maanani ushirikiano wa kilimo na Uganda katika uga wa kilimo nje ya mipaka ya nchi, mafunzo na ushirikiano wa wataalamu na watafiti.
-
Ujumbe wa Algeria na azma yake ya kustawisha ushirikiano wa kiteknolojia na Iran
Apr 30, 2024 07:44Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa Algeria amepongeza maendeleo ya kiteknolojia ya Iran na kusisitiza azma ya nchi hiyo ya kuendeleza ushirikiano wa kiteknolojia na Iran.
-
Iran na nchi za Afrika zaunda kamati ya ushirikiano katika sekta ya kilimo
Apr 29, 2024 23:19Wizara ya Jihadi ya Kilimo ya Iran imetangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika zimekubaliana kuunda kamati ya ushirikiano wa pamoja katika sekta ya kilimo.
-
IRGC: Usaidizi wa nchi 10 duniani kwa Wazayuni haukufua dafu mbele ya Shambulio la Iran
Apr 29, 2024 23:18Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema nchi 10 ziliusaidia utawala wa Kizayuni katika ulinzi wa anga ili kukabiliana na operesheni ya Ahadi ya Kweli ya kuutia adabu utawala huo, lakini hatimaye Iran ya Kiislamu iliisambaratisha na kuishinda mifumo hiyo ya ulinzi ya nchi hizo zinazotajika.
-
Raisi: Mkono wa chuma hauwezi kuzima harakati ya wanachuo Magharibi ya kuunga mkono Palestina
Apr 29, 2024 03:51Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, harakati ya wanafunzi, maprofesa na wasomi wa nchi za Magharibi za kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina ni tukio kubwa lenye muelekeo mipana ambalo haliwezi kuzimwa kwa ukandamizaji, vipigo, kamatakamata na vitendo vya utumiaji mabavu.
-
Raisi: Iran ina ubunifu katika nyanja mbalimbali kwa ajili ya dunia
Apr 27, 2024 09:57Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya sita ya uwezo wa mauzo ya nje ya bidhaa za Iran (Iran Expo 2024) kwamba maonesho haya yanaonyesha kuwa Iran haiwezi kuwekewa vikwazo na ina uwezo wa kufanya uvumbuzi katika nyanja mbalimbali.