Mar 03, 2024 11:14 UTC
  • Utunishaji misuli; Choopan wa Iran atwaa tuzo ya kifahari

Mtunishaji misuli veterani wa Iran, Hadi Choopan ametwaa taji la kimataifa la 'Bwana Olympia' katika tuzo za Arnold Classic 2024.

Fainali ya mashindano ya utunishaji misulu ya Arnold Classic ilifanyika Jumamosi ya Machi 2 katika Ukumbi wa Battelle Grand katika mji wa Columbus jimboni Ohio, magharibi ya Marekani.

Choopan mwenye umri wa miaka 36 ametunukiwa medali ya dhahabu na kitita cha dola 300,000 pesa taslimu baada ya kuibuka kidedea kwenye mashindano hayo ya kimataifa.

Muirani huyo mwenye lakabu ya "Persian Wolf" amempiga na chini bingwa mtetezi Samson Dauda. Choopan ametunukiwa tuzo hiyo ya kifahari na muigizaji maarufu wa Hollywood, Arnold Schwarzenegger.

Bingwa huyo wa utunishaji misuli wa Iran anatazamiwa kurejea mjini Las Vegas jimboni Nevada, kwenye michuano mingine ya 'Mr Olympia' baina ya Oktoba 10 na 13 mwaka huu 2024.

 

Tags