-
Bunge la EU ladhihirisha tena unafiki wa Magharibi kwa kulaani shambulio la kujibu mapigo la Iran dhidi ya Israel
Apr 26, 2024 07:37Bunge la Ulaya limedhihirisha tena sera za undumilakuwili za Magharibi kwa kupitisha azimio la kulaani shambulio la hivi karibuni la kujibu mapigo lililofanywa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuzitolea wito nchi wanachama za umoja huo ziiwekee Tehran vikwazo vingine vipya na vikali zaidi.
-
Amir-Abdollahian: White House inapasa kusitisha haraka uungaji mkono wake kwa jinai za kivita za Israel
Apr 25, 2024 23:39Akikosoa ukandamizaji na unyanyasaji wa askari usalama vya Marekani dhidi ya wahadhiri na wanafunzi wanaopinga jinai za kivita za utawala ghasibu wa Israel, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Ikulu ya Marekani inapasa kusitisha haraka iwezekanavyo uungaji mkono wake kwa jinai za kivita za utawala ghasibu wa Israel.
-
Iran yaitaka UN kukomesha mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza
Apr 24, 2024 23:51Mwakilishi wa Iran katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva amemwandikia barua mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, akiwaomba kuchukua hatua za haraka za kukomesha mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza huko Palestina.
-
Msemaji wa Serikali ya Iran: Kuna Pengo kubwa kati ya viongozi wa Marekani na maoni ya umma
Apr 24, 2024 02:55Msemaji wa Serikali ya Iran amesema, akizungumzia msaada mpya wa kifedha wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, kwamba: Pengo kubwa lililopo kati ya watawala walioathiriwa na Uzayuni na maoni ya umma katika nchi za Magharibi haliwezi kukanushwa tena.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akosoa ufuasi kipofu wa Ulaya kwa Marekani
Apr 23, 2024 08:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuiwekea Iran vikwazo vilivyo kinyume cha sheria, akisema kuwa watu wa Ulaya hawapaswi kufuata ushauri wa Marekani wa kuuridhisha utawala mtendajinai wa Israel.
-
Safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan
Apr 23, 2024 04:54Ziara ya siku mbili ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan inatathminiwa kuwa ni safari ya kihistoria ambayo inatarajiwa kufungua ukurasa na anga mpya ya uhusiano kati ya Tehran na Islamabad.
-
Rais wa Iran asisitiza kukuza ushirikiano wa pande mbili na Pakistan
Apr 22, 2024 23:39Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kukuza ushirikiano kati ya Tehran na Islamabad katika nyanja mbalimbali.
-
Rais wa Iran awasili Pakistan katika ziara ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na usalama
Apr 22, 2024 03:12Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad katika ziara rasmi ya kikazi yenye lengo la kuimarisha usalama na uhusiano wa kibiashara kati ya nchi mbili.
-
Iran yalaani veto ya Marekani dhidi ya uanachama kamili wa Palestina UN
Apr 20, 2024 03:13Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani kura ya turufu ya Marekani dhidi ya rasimu ya azimio iliyotaka Palestina ipewe uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa.
-
Vyombo vya habari: Iran imetungua ndege tatu zisizo na rubani katika mji wa Esfahan
Apr 19, 2024 04:28Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, mfumo wa ulinzi wa anga wa Iran umetungua ndege tatu ndogo zisizo na rubani katika mkoa wa Esfahan ulioko katikati mwa nchi saa kadha baada ya vyombo vya habari vya Marekani kuwanukuu maafisa waandamizi wa nchi hiyo wakidai kwamba makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel yamepiga eneo la Iran.