Apr 24, 2024 06:25 UTC
  • Msemaji wa Serikali ya Iran: Kuna Pengo kubwa kati ya viongozi wa Marekani na maoni ya umma

Msemaji wa Serikali ya Iran amesema, akizungumzia msaada mpya wa kifedha wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, kwamba: Pengo kubwa lililopo kati ya watawala walioathiriwa na Uzayuni na maoni ya umma katika nchi za Magharibi haliwezi kukanushwa tena.

Baada ya mabishano mengi kati ya Wademokrat na Warepublican na hitilafu kubwa zilizotawala baina ya vyama hivyo viwili kuhusu msaada wa kigeni, Baraza la Wawakilishi la Marekani majuzi liliidhinisha kifurushi cha msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 26 kwa ajili ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kura 266 za ndio dhidi ya kura 58 zilizoupinga.

Akizungumzia suala hilo, Ali Bahadori Jahromi, msemaji wa Serikali ya Iran ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba: Bunge la Marekani limeidhinisha kifurushi kipya cha dola bilioni 26 kwa ajili ya kuusaidia utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa: Wakati huo huo vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti habari ya kukamatwa mamia ya wanafunzi nchini humo kwa sababu tu ya kuiunga mkono Palestina.

Ali Bahadori Jahromi

Katika ujumbe wake huo wa mtandao wa kijamii wa X, msemaji wa Serikali ya Iran amesisitiza kuwa: "Pengo kubwa kati ya watawala walioathiriwa na Uzayuni na maoni ya umma katika nchi za Magharibi haliwezi kukanushwa tena."

Tags