May 06, 2024 03:09 UTC
  • Mafuriko Kenya yauwa watu 228

Idadi ya walioaga dunia kutokana na mafuriko yaliyokumba Kenya imeongezeka hadi 228 huku mamlaka husika zikiendelea kukabiliana na tishio la kimbunga Hidaya.

Huku mvua kubwa na upepo mkali ukitarajiwa kuongezeka katika siku zijazo, serikali ya Kenya jana Jumapili iliwataka raia kuchukua tahadhari kubwa kukabiliana na athari za mabadiliko hayo ya tabianchi. 

Isaac Mwaura Msemaji wa serikali ya Kenya jana alieleza kuwa na hapa ninanukuu" Tunaomboleza vifo vya watu 9 katika muda wa saa 24 zilizopita, wakiwemo watu wazima 7 na watoto 2, na kufanya jumla ya vifo vinavyotokana na mafuriko kufikia 228 kote nchini. Serikali inatuma salamu za rambirambi kwa marafiki na familia waliopoteza wapendwa wao." 

Mwaura aliongeza kuwa, cha kusikitisha ni kwamba mafuriko yanayoendelea nchini yamesababisha Wakenya 164 kujeruhiwa huku watu 72 wakiripotiwa kutoweka. Aidha  takriban watu 212,630, kutoka kaya 42,526 wamelazimika kuhama makazi yao."

Mafuriko nchini Kenya 

Kaunti zilizoathiriwa zaidi kwa mafuriko huko Kenya ni pamoja na  Homa Bay, Kajiado, Nakuru, Mandera na Nairobi ambapo zinaendelea kukabiliana na mafuriko makubwa ambayo yamesababisha usumbufu mkubwa kwa maisha ya kila siku na shughuli za kiuchumi.

 

Tags